Flatnews

BRAZIL v ARGENTINA – MESSI NA DI MARIA VS NEYMAR NA OSCAR


BESTPIX-Nigeria-v-Argentina-Group-F-2014-FIFA-World-Cup-Brazil


Na Baraka Mbolembole,
Mechi kubwa zaidi barani Amerika Kusini ni ile inayowahusisha ‘ mabingwa mara saba wa jumla wa kombe la dunia’, nazungumzia Brazil, mabingwa wa dunia wa miaka ya 1958, 1962, 1970, 1994, na 2002, na mabingwa mara mbili wa Argentina. Mechi itakayopigwa mchana huu katika uwanja wa kimataifa wa Beijing, China na itahusisha kikosi cha kocha, Carlos Dunga na Gerlad Martino ambao wote ni makocha waliapewa kazi mara baada ya kumalizika kwa fainali za 21 za Kombe la dunia, Julai, mwaka huu nchini, Brazil. Dunga amechukua nafasi ya Luiz Scolari aliyechemsha katika kombe la dunia, huku Martino akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Sabella ambaye aliisaidia nchi hiyo kufika hatua ya fainali na kupoteza mbele ya Ujerumani kwa kulazwa bao 1-0.
Philipe Coutinho pia ameitwa na anatarajiA kucheza na Oscar, Willian huku wakimzunguka Neymar. Kiungo wa mashambulizi, Elias, 29 ameitwa sambamba na mahambulizi, Diego Tardei, 29. Filipe Luiz, Juan na Danilo wote wameitwa na Dunga na wataungana na mlinzi David Luiz kuisaidia Brazil katika mchezo wa leo
Neymar ameanza kutamba barani ulaya, alifunga mabao 11 katika msimu wake wa kwanza katika La Liga ambao uliambatana na majeraha ya mara kwa mara. Tayari amefunga ‘ hat-trick’ msimu huu na mchezaji huyo amefunga mabao saba katika michezo sita iliyopita. Ameanza kuwasahaurisha mashabiki wa FC Barcelona kuhusu kipaji cha Leonel Messi na pambano la leo litawakutanisha huku kila akiwa amefunga mabao matatu katika michezo sita iliyopita ya mahasimu hao wa soka la Amerika.
BESTPIX-Nigeria-v-Argentina-Group-F-2014-FIFA-World-Cup-Brazil
 AGUERO, MESSI, HIGUAIN, DI MARIA AKITOKEA KATIKATI……
Sergio Aguaro alicheza kwa kiwango cha chini katika kombe la dunia, majeraha yalitajwa kama sababu ya kuvurunda kwake. Alifunga mabao 16 katika ligi kuu ya England wakati akienda katika kombe la dunia, mshambulizi huyo wa mabingwa wa England, Manchester City tayari amefunga mabao matano msimu huu, anategemewa kuanza sambamba na Messi, na Gonzalo Higuain kama, kocha Martino ataichezesha timu yake katika mfumo wa 4-3-3.
Mchezaji bora wa Manchester United kwa sasa, kiungo-mshambuliaji, Angel Di Maria ataanza katika kikosi cha kwanza na anaweza kuwa ‘ mwiba mkali’ kwa safu mpya ya ulinzi ya Dunga. Di Maria alifunga mara moja na kupiga pasi tatu za mwisho wakati, Argentina ilipoichapa, Ujerumani kwa mabao 4-1, mwezi uliopita katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

  neymar-brazil_620-thumb-620xauto-307136
DUNGA ALIMTUMIA MIRANDA , BEIJING ANAMRUDISHA HAPO KUTHIBISHA UWEZO…
Miranda, mlinzi wa kati wa mabingwa wa Hispania, klabu ya Atletico Madrid ameitwa na Dunga. Licha ya kuwa katika kiwango cha juu kwa misimu mitatu sasa, mlinzi huyo ‘ amekwama’ kupata nafasi katika kikosi cha ‘ Wateule 11′, amekuwa akiitwa na wakati mwingine akiachwa kabisa, lakini ili kupata mafanikio atatikiwa kuhimarisha safu ya ulinzi ambayo iliruhusu mabao 13 katika michezo saba ya kombe la dunia, yakiwemo mabao 10 katika michezo ya nusu fainali na ule wa kutafuta mshindi wa tatu wa fainali hizo kubwa zaidi za soka duniani.
Miranda alicheza katika kikosi cha kwanza cha Brazil katika michuano ya Olimpiki, Beijing, 2008 anaweza kupangwa na nahodha, Thiago Silva na kukumbusha enzi wakati, Dunga akiandaa timu ya Brazil kwa ajili ya fainali za kombe la dunia, 2010 nchini, Afrika Kusini. Luiz Fillipe mlinzi wa pembeni wa Chelsea, kiungo wa PSG, Lucas Moura, pia ni baadhi ya machaguo yaliyokosekana katika kikosi cha ‘ Big Phiri’, Dunga amewaita si kwa maana ya kumkosoa kocha aliyepita, bali machaguo hayo yametazama viwango vya nyota hao kwa sasa.
Messi alifunga ‘ hat-trick’ wakati timu hizo zilipozalisha mabao saba katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki, Juni 9, 2012. Argentina ilishinda kwa mabao 4-3. Mshambulizi Fred alifunga bao la kuongoza dakika ya 85, Novemba, 2012 na ilionekana kama bao hilo lingeipatia ubinngwa, Selecao lakini, Ignacio Scocco alisawzisha dakika ya mwisho ya mchezo katika uwanja wa Antonio Vespucio Liberti Ipira, Argentina. Dakika 90 za pambano la mwisho la ‘ Super clasico de las Americas zilimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na Brazil ikitwaa taji la pili kwa mikwaju ya penalti.

Post a Comment

emo-but-icon

item