ALIKIBA AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZA KUKODI WATU WA KUMZOMEA DIAMOND FIESTA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/10/alikiba-afunguka-kuhusu-tuhuma-za.html

Alikiba ameiambia Bongo5 kuwa hajui uvumi huo umeanza vipi.
“Hamna ukweli wowote, naanzaje?,” amehoji. “Siwezi kufanya kitu kama hicho. Kikubwa ni kuwashukuru wana Dar es Salaam walivyonipokea, nimefurahi sana. Hii imenitia moyo na kunifanya niongeze bidii kuwaandalia vitu vizuri zaidi.”
Katika hatua nyingine, msanii huyo amesema mashabiki wa muziki wake wasishangae kuona video ya wimbo wa ‘Mwana’ wiki hii ama wiki ijayo. “Video ni muda wowote yaani, usishangae ukasikia video imetoka. Muda wowote video inatoka surprise, kwahiyo waendelee kusubiri muda wowote.”