UNCDF KUENDELEA KUSAIDIA KUJENGA UWEZO WA KIFEDHA KUHUDUMIA MAENDELEO
https://samchardtz.blogspot.com/2014/09/uncdf-kuendelea-kusaidia-kujenga-uwezo.html
Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt.
Deogratius Mtasiwa, akizungumza kwenye mkutano wa watendaji waandamizi
wa serikali kutoka katika Ofisi ya WaziriMkuu – Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) pamoja na waandishi wa habari kuhusiana
na Programu ya Utafutaji Fedha Nchini kwa maendeleo ya wananchi (Global
Local Finance Initiative (LFI) ambayo ilianza katika awamu ya majaribio
2012 na kuonyesha mafanikio. Kulia ni Mshauri Mkuu wa Ufundi wa
programu hiyo nchini Tanzania , Peter Malika.
Mfuko
wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) umefurahishwa na
programu zinazoendeshwa nchini kwa msaada wake na kusema upo tayari
kuendelea kufanyakazi na serikali na wananchi wa Tanzania.
Kauli
hiyo imetolewa katika ziara ya Katibu Mtendaji wa UNCDF, Judith Karl,
ambaye anaitembelea Tanzania kwenye mkutano wake na watendaji waandamizi
wa serikali kutoka katika Ofisi ya WaziriMkuu – Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) jana.
Karl
ambaye ameongozana na Mkurugenzi wa Local Development Finance kutoka
Makao Makuu ya UNCDF, New York, David Jackson alisema wamefurahishwa
namna Tanzania inavyotekeleza mpango huo wa kuwezesha watanzania
kuchangia miradi yao ya maendeleo kwa kutumia vyanzo vya ndani katika
halmashauri mbalimbali.Miongoni mwa halmashauri zilizofanya vyema ni
Same na Kibaha.
Akiwa
na Mshauri Mkuu wa Ufundi wa programu hiyo nchini Tanzania , Peter
Malika, Mtendaji huyo alisema wamefika kutia saini mkataba wa maelewano
kati ya Tanzania na shirika hilo la Umoja wa Mataifa kwa lengo la
kutekeleza miradi 25 na hasa baada ya awamu ya kwanza wa miradi mitano
kuonesha mafanikio makubwa.
Akizungumza
Karl pamoja na kuelezea kazi za UNCDF nchini Tanzania alitangaza
kuanzishwa kwa Programu ya Utafutaji Fedha Nchini kwa maendeleo ya
wananchi (Global Local Finance Initiative (LFI) kwa mwaka 2014-2017,
ikiwa ni jitihada mpya ya UNCDF iliyoanzishwa kufuatia maarifa
yaliyopatikana katika utekelezaji wa LFI ya kwanza (Tanzania) katika
awamu ya majaribio (2012-2015).
Katibu
Mtendaji mpya wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa
(UNCDF), Bi Judith Karl akizungumza na baadhi ya wajumbe wa TAMISEMI
pamoja na waandishi wa habari juu Programu ya utafutaji fedha nchini kwa
maendeleo ya wananchi (Global Local Finance Initiative (LFI), ambapo
alitangaza kuizindua rasmi program hiyo katika mkutano uliofanyika
kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OWM-TAMISEMI). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu – OWM-TAMISEMI, Dkt.
Deogratius Mtasiwa.
Hadi
sasa, programu ya majaribio ya LFI nchini Tanzania inasaidia miradi 25
ya miundombinu iliyoanzishwa na wawekezaji wa umma na binafsi na ambayo
iko katika hatua mbalimbali za uendelezaji. Lengo la programu hiyo ni
kuanzisha makampuni makubwa ya uwekezaji katika halmashauri ili
kupunguza mchango wa serikali kuu katika mambo ambayo yanaweza kufanywa
na wananchi na wao wakabaki katika sera na mipango mikubwa.
Miradi
imetawanyika katika sekta mbalimbali zikiwezo za usindikaji bidhaa za
kilimo, nishati, miundombinu ya utoaji huduma za jamii, mawasiliano, na
uzalishaji viwandani, katika mikoa 10 kote nchini.
Miradi
mitano iliyopiga hatua kubwa zaidi inatarajiwa kufikia kikomo cha
bajeti yake katika miezi sita hadi tisa ijayo ambapo dola milioni 26 za
mtaji wa ndani katika muundo wa mkopo na misaada ipatayo dola milioni 3
ilihamasishwa.
Msaada
wa LFI kwa miradi ambayo iko katika muundo wa utaalamu wa kiufundi,
kutoa amana, misaada ya kifedha , mikopo ambayo inahitajika sana kwa
miradi midogo na ya kati ya miundombinu ili ivutie uwekezaji.
Matokeo
ya jumla ya LFI ni kuongezeka kwa ufanisi wa rasilimali fedha kwa ajili
ya maendeleo ya kiuchumi ya hapa nchini kupitia uhamasishaji kwanza
kabisa wa mtaji binafsi kutoka nchini na masoko ya mitaji ilikuwezesha
na kuhamasisha maendeleo ya mahali yaliyojumuishi na endelevu.