UMOJA WA VIJANA WAZALENDO WA VYUO VYA ELIMU YA JUU DAR ES SALAAM WATOA TAMKO LA KULAANI KAULI ZA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA KWA MADAI YA KUHAMASISHA MAANDAMANO
https://samchardtz.blogspot.com/2014/09/umoja-wa-vijana-wazalendo-wa-vyuo-vya.html
Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana Wazalendo wa Vyuo vya Elimu ya Juu Mkoa wa Dar es
Salaam, Mussa Omary, akisoma tamko hilo, Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana Wazalendo wa Vyuo vya Elimu ya Juu Mkoa wa Dar es
Salaam, Mussa Omary (katikati), akizungumza na waandishi wa habari
wakati akisoma tamko hilo. Kulia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM), Theodora Malata na Mwanachuo Chuo cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere, Rehema Akukweti.
Wawakilishi wa wanafunzi wa vyuo vikuu 12 vya Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Mwanachuo
wa UDSM, Gulatone Masiga akijibu maswali ya waandishi wa habari.
Kushoto ni Mwanachuo Mwita Nyarukururu na Mwenyekiti wa umoja huo, Mussa
Omary.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Theodora Malata, akichangia jambo wakati wa kujibu maswali ya wanahabari.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanachuo
Mussa Mashamba kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii, akisisitiza jambo
wakati akijibu maswali ya wanahabari. Kulia Massoro Kivuga na William
Haule. Dotto Mwaibale
UMOJA
wa Vijana Wazalendo wa Vyuo Vikuu 12 vya Mkoa wa Dar es Salaam,
wamemshukia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)
Freeman Mbowe kwa kutaka kuitisha maandamano ya kupinga Bunge Maalum la
Katiba.
”Sisi umoja wa vijana wa vyuo vikuu tunapinga vikali kauli hiyo na kulaani vikali ya kuhamasisha uasi kwa njia ya maandamano,”alisema.
”Sisi umoja wa vijana wa vyuo vikuu tunapinga vikali kauli hiyo na kulaani vikali ya kuhamasisha uasi kwa njia ya maandamano,”alisema.
Akizungumza
Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa vijana hao Mussa Omary alisema kauli
aliyotoa mwenyekiti huyo inahamasisha kuleta mgogoro nchini.
”Tumesononeshwa
na kauli hiyo ya kibabe ya kiongozi huyu ya kuhamasisha vurugu ambazo
tumezishuhudia zikisambaratisha umoja wa nchi nyingi na kuwa chanzo cha
vita,”alisema.
”Tulimsikia
akiahidi maandamano bila kikomo kwa kibali cha polisi au hata bila
kibali cha polisi mbele ya wajumbe ambao wengine sio watanzania,”
Omari alisema uzito wa jambo hilo unaonesha wazi kuwa Mwenyekiti huyo hasatahili hata kidogo kuweza kupewa uongozi wa nchi hii.
Aliongeza
kuwa mwenykiti huyo na viongozi wenzakae wanatumia maandamano na damu
za watanzania kutafuta fedha kwa wafadhili wao ambao hawaitakii nchi hii
mema.
”Wakiandaa maandamano haya huwa wanapiga picha na kuwatumia wafadhili wao na kupata fedha na kujenga majumba na kununua magari makubwa na huku watanzania wakiendela kuathirika,”alisema.
”Wakiandaa maandamano haya huwa wanapiga picha na kuwatumia wafadhili wao na kupata fedha na kujenga majumba na kununua magari makubwa na huku watanzania wakiendela kuathirika,”alisema.
Alisema
thamani ya mtanzania mmoja ni kubwa kuliko hiyo katiba mpya wanayodai
ni vizuri watanzania kuacha kuwaunga mkono na kufanywa kama mbuzi wa
kafara.
Aliongeza
kuwa ni vyema vyombo vya dola visiweze kuvumilia kauli hiyo iliyotolewa
hivyo kuendelea,kulinda kutunza na kuweza kuiendeleza amani ya nchi.
”Ni
vizuri watanzania wakakaa na kufikiria kauli hii ya mwenykiti huyu na
kujiuliza kuwa je ni kweli anaweza kuwa kiongozi wa nchi hii,”alisema.
Naye,mmoja
wa wanafunzi hao Theodera Nalaya alisema ni vizuri tukaliachia bunge
maaluma likafanya kazi yake ya kutafuta katiba mpya.
”Sisi kama vijana wa vyuo vikuu msimamo wetu ni kuwa tuliachie bunge la katiba likafanya kazi yake na muda ukifika wa kutoa maoni yetu ukifika tutatoa maoni yetu na si kuvamia,”alisema.
”Sisi kama vijana wa vyuo vikuu msimamo wetu ni kuwa tuliachie bunge la katiba likafanya kazi yake na muda ukifika wa kutoa maoni yetu ukifika tutatoa maoni yetu na si kuvamia,”alisema.