Flatnews

News alert: Watatu Wapoteza Maisha Zaidi ya 60 Wajeruhiwa Kwa Mabomu kwenye mabasi ya abiria nairobi leo

Watu watatu wamepoteza maisha na wengine 62 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka Jumapili ya leo katika barabara ya Thika, am...



Watu watatu wamepoteza maisha na wengine 62 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka Jumapili ya leo katika barabara ya Thika, ambayo ni moja ya njia kuu zenye magari mengi jijini Nairobi, Kenya.Majeruhi 20 kati ya hao wako mahututi.



Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi la Kenya Bw. Moses Ombati amenukuliwa akisema kuwa  mabomu hayo yamelipuka kwenye mabasi ya abiria mawili tofauti, ambapo Naibu Mkuu wa kitengo cha kutengua Mabomu, Bw, Eliud Lagat amesema milipuko hiyo imetokana na mabomu yaliyotengenezwa kienyeji.


Milipuko hiyo na maafa hayo yamekuja siku moja baada ya watu wanne kuuwawa kwa mlipuko wa bomu ya kutupwa kwa mkono katika kituo cha mabasi mjini Mombasa. Mlipuko mwingine katika ufukwe wa bahari haukuleta madhara.




Kenya imekumbwa na wimbi la mashambulio ya bunduki na milipuko ya mabomu toka nchi hiyo ilipopeleka majeshi yake kupambana na wanaodaiwa kuwa wafuasi wa kundi la kigaidi la Al-Shabab mwaka 2011, ambao wameapa kuendeleza mashambulio ya kigaidi kama kulipiza kisasi kwa kuwepo kwa majeshi ya Kenya nchini Somalia.


Post a Comment

emo-but-icon

item