AS Roma yaichapa CSKA Moscow mabao 5-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya
https://samchardtz.blogspot.com/2014/09/as-roma-yaichapa-cska-moscow-mabao-5-1.html
mkongwe
wa umri wa miaka 37, Francesco Totti wamefanya kazi nzuri usiku huu
AS Roma ikiifumua CSKA Moscow mabao 5-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya
Uwanja wa
Olimpico.
Gervinho
amefunga mabao mawili na kuseti lingine moja lililofungwa na mchezaji
mpya, Juan Iturbe wakati mabao mengine yamefungwa na Maicon na Totti,
wakati bao pekee la CSKA limefungwa na Ahmed Musa.
Bahati mbaya kwao Roma, Iturbe aliumia
kipindi cha kwanza na kutoka.
Katika michezo mingine, Athletic Bilbao
imelazimishwa safe ya 0-0 na Shakhtar
Donetsk wakati Porto iliichapa 6-0 BATE jana.
