MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF AFANYA MAZUNGUMZO YA AWALI KUHUSU UWEKEZAJI KATIKA MAENEO YA JESHI LA MAGEREZA MKOA WA DAR ES SALAAM NA MTWARA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/08/mkurugenzi-mkuu-wa-mfuko-wa-pensheni-wa.html
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akiongoza Kikao
cha Mazungumzo ya Awali na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,
Bw. William Erio(hayupo pichani) kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya
Jeshi la Magereza Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio akifanya mazungumzo
ya Awali na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir
Minja(hayupo pichani) kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la
Magereza Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara leo Agosti 11, 2014 Jijini Dar
es Salaam.
Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia mazungumzo ya Awali na
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw William Erio(hayupo pichani) kuhusu Uwekezaji
katika maeneo ya Jeshi la Magereza Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara(wa
kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa(katikati) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(Kushoto)
ni Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Solomon Urio akifuatilia
kwa makini mazungumzo hayo.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto)
akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William
Erio eneo linalofaa Uwekezaji wa Hoteli kubwa ya Kimataifa lililopo
Ukonga, Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa PPF amefanya mazungumzo ya
Awali na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza kuhusu Uwekezaji katika
maeneo ya Jeshi la Magereza leo Agosti 11, 2014 Jijini Dar es Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini John Casmir Minja akiagana na
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio(kulia)
mara tu baada ya kufanya mazungumzo ya Awali kuhusu Uwekezaji katika
maeneo ya Jeshi la Magereza katika Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF amefanya mazungumzo hayo leo Agosti 11, 2014
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam(Picha zote na
Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).