Je, hiki kitu ni kweli kumhusu mwigizaji JB?
https://samchardtz.blogspot.com/2014/08/je-hiki-kitu-ni-kweli-kumhusu-mwigizaji.html
Kutoka kwenye mtandao maarufu wa habari nchini - BongoClanTz tumekutana na ujumbe huu unaomlenga msanii nguli nchini Jacob Steve ama JB kama wengi wanavyopenda kumuita.
Ujumbe huu ni kuhusu kazi zake mbalimbali za filamu anazozifanya mwigizaji huyu. Na unasomeka kama ifuatavyo’-
“Mimi sio mpenzi sana wa kuangalia filamu, ila mara chache tu huwa naangalia hasa kwenye mabasi ninaposafiri.
Kitu kinachonikera kwenye hizi Bongo movie hasa za JB ni kutumia wahusika wale wale na theme ile ile mwisho ana bore sasa.
Mfano ni huyu Shamsa Ford, huwezi kuangalia picha ya JB usimkute, tena kwenye filamu hiyo lazima ataishia kuolewa na JB.
Ni kweli Shamsa ni mzuri, lakini kwani yuko pee yake kwenye filamu?
Halafu kwa nini theme iwe mapenzi tu?
Nachoka kabisa" Alimaliza mdau..
Vipi wewe mdau? Una maoni gani kuhusu maoni hata ya mdau huyu wa filamu?