Wahamiaji wafariki Utaliana
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/wahamiaji-wafariki-utaliana.html
Taarifa kutoka Utaliana
zinaeleza kuwa wafanya kazi za uokozi wamekuta maiti 19 kwenye mashua
iliyowabeba mamia ya wahamiaji kutoka Afrika Kaskazini.
Shirika la habari la Utaliana, ANSA, linasema
inavoelekea wanyonge hao walikosa hewa safi walipogubikwa na moshi wa
injini kongwe chini ya deki.Wahamiaji wawili kwenye mashua hiyo walinusuriwa kwa helikopta kupelekwa hospitali.