KAPOMBE AWAANGUKIA WATANZANIA AKITAKA WAJITOKEZE KWA WINGI KUISHANGILIA TAIFA STARS IKIICHAKAZA MAMBAS
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/kapombe-awaangukia-watanzania-akitaka.html
KIUNGO
na beki wa timu ya Taifa ya Tanzania, Shomary Kapombe amewaomba
watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao dhidi ya Msumbiji
`Black Mambas` katika mechi muhimu ya kuwania kupangwa hatua ya makundi
ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika, AFCON,
mwakani nchini Morocco.
Mchezaji
huyo kiraka alisema wachezaji 11 wanaocheza uwanjani hawatoshi kupata
ushindi, hivyo mashabiki kama wachezaji wa 12 wanatakiwa kujitokeza kwa
wingi kuishangilia Taifa Stars.
“Napenda kuwaambia watanzania wote kuwa huu ni mchezo muhimu, nawaomba watanzania waje kuisapoti timu”. Alisema Kapombe.
Aidha,
Kapombe aliongeza kuwa kambi waliyoweka Mjini Tukuyu mkoani Mbeya
imekuwa ya mafanikio kwasababu wachezaji wote wapo katika morali ya
kufanya vizuri katika mchezo wa kesho.
Kapombe alisema kocha Mart Nooij amewabadili katika baadhi ya mambo kiuchezaji na ufundi licha ya kukaa na timu kwa muda mfupi.
Aliongeza kuwa kocha Nooij alikuwa anakazania zaidi safu ya ulinzi kwasababu ndio inafanya kazi kubwa zaidi katika mchezo.
Taifa
stars inahitaji kuifunga Msumbiji si chini ya mabao 3-0 ili kujiweka
vizuri kuelekea mchezo wa marudiano utakaopigwa mjini Maputo nchini
Msumbiji.
Mwaka
2007, Mambas waliifunga Stars bao 1-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu
fainali za AFCON mwaka 2008 nchini Ghana na mechi hiyo ilipigwa ndani ya
dimba la Taifa.
Miaka
miwili iliyopita, Stars ililazimishwa sare ya bao 1-1 katika dimba la
Taifa na kwenda kutoa sare nyingine Mjini Maputo, lakini kikosi hicho
kilichokuwa chini ya kocha Kim Poulsen kiliondolewa kwa mikwaju ya
penati.
Mechi hiyo ilikuwa ni kuwania tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2013 nchini Afrika kusini.