DEREVA WA BODABODA ANUSURIKA KIFO KWA WIZI WA SIMU
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/dereva-wa-bodaboda-anusurika-kifo-kwa.html
Dereva wa bodaboda anayetambulika kwa jina la Abuu Athumani (28) mara baada ya kunaswa kwa wizi wa simu.
Ule
mchezo wa kukwapua vitu na kukimbia umemtokea puani dereva wa pikipiki
almaarufu bodaboda aliyetambulika kwa jina la Abuu Athumani (28) ambaye
amenusa kifo baada ya kukwapua simu ya bei mbaya ya mrembo aitwaye
Zaituni Hamisi.Tukio
hilo la aina yake lilijiri majira ya asubuhi wikiendi iliyopita maeneo
ya Sinza-Mapambano, Dar ambapo kwa mujibu wa mashuhuda bodaboda huyo
alikuwa amempakiza mwenzake kisha kumfuatilia mrembo huyo kwa nyuma
wakati akitembea kwa miguu pembezoni mwa Barabara ya Shekilango.
Dereva huyo wa bodaboda akiwa kwenye mtaro na pikipiki yake mara baada ya kipigo kutoka kwa wananchi.
Shuhuda
huyo alisema kuwa alishangaa kumuona yule jamaa aliyepakizwa akimkwapua
mrembo huyo lakini kwa bahati nzuri mmoja wa madereva wa Bajaj aliyekuwa
karibu alimuona na kumbananisha pembezoni mwa barabara na hatimaye
kuingia mtaroni.Raia walioshuhudia mkasa huo wakiitoa bodaboda kutoka mtaroni.
Ndani ya dakika sifuri, yule mkwapuaji alitoka nduki huku akimwacha bodaboda huyo aliyekiona cha moto.Kulia ni mrembo(Zaituni Hamisi) aliyekwapuliwa simu yake na waendesha bodaboda hao.
Alisema
ghafla umati ulijaa na kushuhudiwa akipewa kipondo cha kufa mtu na
wengine wakidai kuwa ni kawaida ya jamaa huyo kukwapua mikoba ya
watu.Baadhi ya watu walikuwa wakichanga fedha kwa ajili ya kununua
mafuta ya petroli ili wamchome moto bila kujali polisi aliyefika ambaye
alikuwa akijitahidi kutuliza ghasia hizo.
Dereva huyo wa bodaboda akichukuliwa na Polisi mara baada kunusullika kifo kutoka wa raia wenye hasira kali.
Wakati
akipewa kipigo, njemba huyo alikuwa akilalamika na kuwaomba wananchi
wasimuue kwani amekoma na hatarudia tena.Hata hivyo, bodaboda huyo
alinusurika baada ya polisi wa Kituo cha Kijitonyama (Mabatini) kufika
eneo hilo kisha kumchukua jamaa huyo na mlalamikaji kwa ajili ya hatua
za kisheria.
Imeandaliwa na Chande Abdallah,