Beckham kurejea uwanjani
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/beckham-kurejea-uwanjani.html
Aliyekuwa mchezaji wa Uingereza
na Manchester United David Beckham amedokeza kuwa huenda akarejea
uwanjani akiichezea timu yake inayoshiriki ligi kuu ya Marekani MLS
Major League Soccer huko Miami.
Nahodha huyo wa zamani wa Uingereza 39 alistaafu mwezi Mei 2013 baada ya kucheza kwa miaka 20 iliyokamilikia Paris St-Germain.Beckham
"1992-2003: Manchester United 1994-1995: Preston North End 2003-2007: Real Madrid 2007-2012: Los Angeles Galaxy 2009-2010: AC Milan 2013: Paris St-Germain 1996 - 2010: Uingereza"
Beckham anasema kuwa amepumzika vya kutosha na kuwa anapania kurejea uwanjani siku moja ,akijiuliza baada ya kutizama mechi za mpira wa vikapu iwapo anaweza kurejelea hali ya ushindani hata baada ya kustaafu.
Aliwahi kuichezea Uingereza katika mechi 115.
Katika kandarasi yake alipokuwa akiichezea timu ya Los Angeles Galaxy Beckham alitia sahihi kipengee kinachomruhusu kununua timu moja katika ligi hiyo kwa pauni milioni £25m na sasa anaazimia kuzindua klabu huko Miami katika msimu wa 2016 ama 2017.