Wanajeshi wawili wa DRC jela kwa ubakaji
Wanajeshi wa DRC
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/wanajeshi-wawili-wa-drc-jela-kwa-ubakaji.html
Wanajeshi wawili wa Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo wamepatikana na hatia ya ubakaji kati ya wanajeshi
39 walioshitakiwa kwa makosa ya kivita mashariki mwa nchi hiyo.
Wengine waliobaki wamepunguziwa makosa kutoka
makosa ya uhalifu wa kivita lakini wamehukumiwa kwa makosa mengine kama
vile uporaji lakini wengi waliachiwa.Wakati wa machafuko hayo maelfu ya wajeshi wa serikali walikuwa wakirudi nyuma baada ya kupoteza mji wa Goma kwa waasi wa M23 .
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa wanajeshi hao waliwabaka karibu wanawake na wasichana 135.
Matukio ya ubakaji yameenea katika eneo la mashariki mwa Congo na yanaidiwa kufanywa na askari wa pande zote mbili waasi na wale wa serikali.