Uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kwa ajenda ya maendeleo baada ya 2015:UM
...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/uhuru-wa-vyombo-vya-habari-ni-muhimu.html?m=0
Jana
tarehe 3 Mei, 2014 ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, Umoja
wa Mataifa na shirika lake la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO
umesema mafanikio ya utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu baada
ya mwaka 2015 kunategemea haki ya msingi ya raia ya kutoa maoni yao na
kujieleza.
Taarifa
ya pamoja ya Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina
Bokova imesema haki hizo ni muhimu ili kuwepo kwa demokrasia, uwazi,
uwajibikaji na utawala wa kisheria kwani mambo hayo ni muhimu kwa utu wa
binadamu, maendeleo ya kijamii, ushirikishi na maendeleo.
Wamesema
hata wakati huu ambapo dunia imeelekeza jitihada zake kwenye maendeleo
baada ya mwaka 2015, ni vyema kukabiliana na vitisho dhidi ya uhuru wa
vyombo vya habari duniani kote. Mathalani wamesema watendaji wa vyombo
vya habari wanakabiliana na vikwazo vya kimfumo wanapotaka kuripoti
ukweli ikiwa ni pamoja na kubinywa uhuru wao, kukamatwa na kutishiwa
uhari wao na mara nyingine kuuawa.
Ban
na Bokova wamesama utawala bora utakuwepo tu pale ambapo waandishi wa
habari watakuwa huru kufuatilia na kuchunguza na hata kukosoa sera na
vitendo mbali mbali.
Wamesema
wakati vyombo vya Umoja wa Mataifa vikishirikiana na wadau wake chini
ya uongozi wa UNESCO kuweka mazingira huru na salama kwa waandishi wa
habari duniani kote, ni vyema siku ya leo serikali, jamii na kila mtu
mmoja mmoja kutetea na kulinda uhuru huo kwani ni haki ya msingi na ina
nafasi kubwa katika kufanikisha malengo ya milenia na ajenda endelevu
baada ya mwaka 2015. (CHANZO: UM RADIO) (FS)