Flatnews

Shambulio la sokoni Uchina lawaua 31


Shambulio katika mji wa Urumqi
Polisi katika eneo la shambulio kwenye soko la Urumqi lililowauwa watu 31
Washambuliaji wamevamia soko moja na kugonga magari mawili ya wanunuzi katika jimbo la Uchina la Xinjiang , na kuwauwa watu 31, vimearifu vyombo vya habari vya Uchina .
Pia walirusha vilipuzi wakati wa shambulio katika jimbo la mji mkuu wa jimbo hilo Urumqi. Zaidi ya watu 90, wamejeruhiwa , lilieleza shirika lahabari la kitaifa Xinhua.
Waziri wa usalama wa umma aliyataja mashambulio hayo kama "tukio la ghasia za ugaidi".
Jimbo la Urumqi, ambalo linakaliwa na jamii ya waislam walio wachache wa Uighur , limekuwa likikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara mwaka uliopita.
Mwezi uliopita shambulizi la bomu kwenye kituo cha mafuta mjini Urumqi liliwauwa watu watatu na kuwajeruhi wengine kadhaa . Uchina inawalaumu waislam wa jamii ya Uighur wanaotaka kujitenga kutekeleza mashambulio hayo.
Uhasama baina ya jamii za kichina za Uighur na Han unaoendelea, unadhibitiwa.
"Walioshuhudia tukio hilo wanasema magari mawili aina ya cross-country yaliyokuwa yakiendeswha kutoka kaskazini kuelekea kusini yaliingia kwenye umati wa watu waliokuwa sokoni saa 07:50. Halafu madereva wakatupa vilipuzi nje ya gari ," limeripoti shirika la Xinhua .
Maafisa katika mji mkuu wa uchina Beijing wametangaza kuchukuliwa kwa hatua za usalama katika maeneo 14 muhimu.

Post a Comment

emo-but-icon

item