RAMBIRAMBI MSIBA WA MKUFUNZI KASINDE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Mkufunzi wa waamuzi nchini, Omari Kasinde kilichotokea ...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/rambirambi-msiba-wa-mkufunzi-kasinde.html
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea
kwa masikitiko kifo cha Mkufunzi wa waamuzi nchini, Omari Kasinde kilichotokea
jana (Mei 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Mbali
ya kuwa Mkufunzi, Kasinde ambaye anazikwa leo (Mei 13 mwaka huu) mchana katika
Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam pia alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati
iliyopita ya Waamuzi ya TFF iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Kapteni mstaafu
Stanley Lugenge.
Msiba
huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini kwani, Kasinde enzi za uhai
wake alitoa mchango mkubwa katika mchezo huu tangu akiwa mwamuzi na baadaye
mkufunzi na kiongozi..
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kasinde, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Dar es Salaam (DRFA), na Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na
kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo
mzito.
Bwana
alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)