NAMISS SANA WEMA, HAKIKA KWANGU ALIKUWA ZAIDI YA RAFIKI - KAJALA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/namiss-sana-wema-hakika-kwangu-alikuwa.html
“Good
morning all of You…. I just woke up Like “Hasiraless” kwakuwa hili vugu
vugu la kutokuwa na maelewano mazuri kati ya Wema sepetu (myclient) na
Kajala limekuzwa katika social networks basi na mimi naomba nitoe
taarifa kutoka kwetu endless fame.
Katika
urafiki kuna mengi yanajitokeza na endapo kutakuwa na hitilafu sehemu
basi ni muhimu kupeana nafasi ili kila mtu aweze kujirekebisha na mwisho
wa siku maisha yaendelee hilo ndo lililotokea baina ya hawa wawili.
Lakini katika kipindi hicho cha so called mapumziko kuna mambo mengi
yamejitokeza, yapo ya kweli na yapo yaliyotengenezwa na baadhi ya watu,
kuna media coverage juu ya hawa wawili na wema sikumpa nafasi ya
kuzungumza na chombo chochote cha habari kwakuwa nilijua litakuzwa
zaidi… ila tulipoona shutuma zinazidi kuja upande wake akafanya
interview na gazeti moja na kuelezea upande wake na mwisho alisema hana
tatizo na kajala sema tu Kwa sasa anahitaji space
… tukawa tumefunga mjadala huo.
… tukawa tumefunga mjadala huo.
Endless
fame(wema sepetu) haijawahi kutamka lolote swala la mahusiano ya kajala
na mtu yoyote, EndlessFame haijawahi kudoubt urafiki wa kajala na any of
her friends because tunaamini yale ni maisha yake binafsi na
hayahusiani na kampuni ya wema au wema mwenyewe, kusaidiana katika
matatizo haimaanishi tunammiliki… hapana hapana… Hili linaloendelea sasa
sisi pia tumelisikia na kuliona kwenye social networks kama watu
wengine wanavyoona.
Tunaumizwa
na blogs na magazeti yanapoandika stori kama vile wanaushahidi kutoka
endless fame au Kwa mtu wa karibu na wema. Team wema wote waliopo insta
sijawahi kuona hata mmoja kati yao hivyo hakuna anayewatuma wala
kuwashinikiza ila wao wanafanya kile kinachowapendeza and hatuwezi
kuwakataza kwasababu ni maisha yao binafsi na ni mapenzi yao ya dhati
Kwa wema.
Poleni
Kwa wote mnaoumizwa na haya yanayoendelea ila nadhani tukazane na kazi
zetu na maisha yetu maana haya ya instagram tuwaache huku huku
ukiyasikiliza utashindwa kumwamini mama yako mzazi.”
Hivi
karibuni Kajala alisema kutokana na jinsi ambavyo ugomvi wake na Wema
Sepetu ulivyokuwa mkubwa, amefikia hatua anaigopa simu yake zaidi ya
kupiga na kupokea.
Akiongea
kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV wiki hii, Kajala alisema
amekuwa akiumizwa na jinsi anavyotukanwa kwenye mitandao ya kijamii
kutokana na ugomvi huo. Kajala amesema ugomvi wake na Wema haujatokana
na kile kinachodaiwa kuwa alimchukulia ‘bwana yake’ na kwamba umetokana
na vitu vidogo ambavyo ni binafsi kwao. Alidai kuwa pamoja na ugomvi wao
kusababisha na mambo ya kawaida, umekuzwa mno na watu pamoja na vyombo
vya habari kiasi cha kuwafanya wajikute maaudui kweli.
Kuhusiana
na tetesi kuwa alianza kumdharau Wema baada ya Miss Tanzania huyo wa
zamani kuishiwa fedha, Kajala amesema amekuwa rafiki yake tangia enzi
hana chochote. “Alikuwa rafiki yangu kabla hana kitu, kwahiyo kwamba
nilianzisha urafiki na Wema kwasababu alikuwa na hela lakini sasa hivi
hana hela mimi sio rafiki yangu tena, sio kweli,” alisema.