MABONDIA SAID MBELWA, KARAMA NYILAWILA KUPANDA ULINGONI MEI 24 MANZESE
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/mabondia-said-mbelwa-karama-nyilawila.html
Mabondia Karama Nyilawila kushoto na
Said Mbelwa wakitambiana wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa
kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frende corner manzese
katikati ni katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini PST Antony
Rutta picha nawww.superdboxingcoach. blogspot.com
Mabondia Karama Nyilawila kushoto na
Said Mbelwa wakitambiana wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa
kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frende corner manzese
picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com
Mabondia Karama Nyilawila kushoto na
Said Mbelwa wakitambiana wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa
kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frende corner manzese
picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Said Mbelwa na Karama
Nyilawila wametambiana kila mmoja kuibuka mbabe katika mpambano wao wa
kugombania ubingwa wa Univers Boxing Oganaization UBO mpambano
utakaofanyika katika ukuimbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam
likiwa linasimamiwa na chama cha ngumi
za kulipwa nchini PST mpambano huo utakao onesha kuwa nani mbabe wa
uzani wa kg 76 ubingwa wa UBO akizungumzia mpambano huo Katibu mkuu wa
shilikisho la ngumi za kulipwa nchini Antony Rutta amesema kuwa mpambano
huo unaosubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi nchini ukuiwa na
mabondia wote wamecheza ngumi za kitaifa na kimataifa yani ndani na nje
ya nchi
akitolea mfano bondia Said Mbelwa ndie
bondia pekee ambaye anaenda nje ya nchi kucheza ngumi na kumaliza raundi
zote 12 walizo pangiwa ingawa anapigwa kwa pointi ambapo mabondia wengi
wa Tanzania wakienda nje wanapigwa K,O mbaya sana ambazo zinawatia
mpaka itrafu katika baadhi ya maeneo
akimzungumzia Nyilawila ambaye alikuwa
bingwa wa dunia wa uzani huo wa WBF ambaye alichukua mkanda huo nje ya
nchi jambo ambalo kubwa sana duniani kumpiga mzungu nyumbani kwao si
mchezo hivyo mabondia wote hawa wana sifa zinazo lingana
nae bondia Mbelwa aliongeza kwa kusema
kuwa mimi nipo fiti hivyo mashabiki waje kwa wingi kuangalia ngumi
ambazo zitahacha historia kubwa katika jiji la Dar es salaam na
vitongoji vyake kwa kipigo nitakachompa Karam
Katika mpambano huo siku hiyo
kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na
kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile gem ya fransic
Miyeyusho vs Mohamed Matumla 'Sneak jr' mpambano ulivuta hisia za
wapenzi wengi wa ngumi nchini
