KIZAAZAA: PEMBE, SENGA WAVURUGA MTAA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/kizaazaa-pembe-senga-wavuruga-mtaa.html
Stori: Mwandishi Wetu, Kahama
WASANII nyota wa vichekesho Bongo, Ulimboka Mwalulesa ‘Senga Kijumule’ na swahiba wake, Yusuph Kaimu Machoti ‘Pembe’ hivi karibuni walifunga mtaa mjini Kahama baada ya mashabiki kuwazunguka kwa dakika 45 wakiwashangaa.

Wawili hao ambao walijipatia umaarufu mkubwa wakati walipokuwa wakiigiza kupitia televisheni, walikuwa katika Wilaya za Mbogwe na Kahama wakati wa uzinduzi wa albamu ya tatu ya msanii wa muziki wa asili wa Kabila la Wasukuma aitwaye Bhudagala.
Baada ya wananchi kuwaona wasanii hao wakitembea kwa miguu katika mitaa mjini hapa, walianza kuwafuata taratibu na hatimaye kujikuta wakiwa kundi kubwa ambalo halikutarajiwa.