JK,SHEIN NDIYO WANAOWEZA KUIREJESHA UKAWA BUNGENI"
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/jkshein-ndiyo-wanaoweza-kuirejesha.html
Dar
es Salaam. Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Juma
Duni Haji amesema watu pekee wanaoweza kulinusuru kundi la Umoja wa
Katiba ya Watanzania (Ukawa), kurejea bungeni ni Rais Jakaya Kikwete na
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.Duni
ambaye pia ni kiongozi wa CUF, alisema hayo jana kwenye mdahalo kuhusu
Bunge Maalumu la Katiba tunayoitaka uliofanyika Dar es Salaam.Ngoma
hiyo imeshakwama, kamwe haturudi bungeni kujadili mambo ya CCM kwani
hayatuhusu. Kwa mazingira yaliyopo, ule sasa umegeuka kuwa mkutano wa
Halmashauri Kuu ya CCM, wanaweka mambo yenye masilahi kwa chama chao,
kamwe haturejei,” alisema.Alisema
kama viongozi hao hawazioni dosari zinazofanywa na wajumbe wa CCM, basi
suala la kupata Katiba Mpya ni ndoto kwa sababu Ukawa hawako tayari
kurejea katika Bunge hilo.
“Tunawaachia CCM waandae Katiba ya Watanzania, sisi hatutashiriki kwa sababu tumegundua rafu hiyo mapema,” alisema.
Hata
hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema hata
kama Ukawa hawatarejea bungeni, vikao vitaendelea kama kawaida kwa
sababu kanuni zinawaruhusu kufanya hivyo.
“Katika
Bunge Maalumu la Katiba, wapo wabunge wa CCM na wale 201. Walioteuliwa
na Rais ambao walitoka nje pamoja na Ukawa ni wajumbe 25 na wamebaki
176, hivyo watu wasiseme waliobaki ni wajumbe wa CCM,” alisema.