JESHI LA POLISI MBEYA LAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA MAUAJI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/jeshi-la-polisi-mbeya-lawashikilia-watu.html
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 22.05.2014.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWSHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA MAUAJ1.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO KWA KUKUTWA NA FUNGUO BANDIA 203.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA WATU WATATU KWA KUKUTWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] NA MTAMBO MMOJA.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWAFIKISHA MAHAKAMANI WATU WANNE KWA KUFANYA BIASHARA SEHEMU ISIYORUHUSIWA.
TUKIO LA KWANZA.
JESHI LA POLISI MKOA WA LINAWSHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA ZA MAUAJ1.
JESHI
LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WA FAMILIA MOJA JERI KAPONDA [22]
NA ROGER KAPONDA [19] WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ISUTO WILAYA YA
MBARALI KWA KOSA LA MAUAJI.
AWALI
TAREHE 18.05.2014 MAJIRA YA SAA 22:00HRS USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA
ISUTO, KATA YA CHIMALA, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI
WATUHUMIWA WALIMSHAMBULIA BAHATI SANGA [40] MKAZI WA KIJIJI HICHO KWA
KUMPIGA FIMBO,NGUMI NA MATEKE TUMBONI NA KIFUANI KISHA KUMFUNGIA NDANI
YA NYUMBA YAO HADI TAREHE 20.05.2014 ALIPOFANIKIWA KUTOROKA NA KWENDA
KUTOA TAARIFA POLISI NA BAADAE KULAZWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA
HADI ALIPOFARIKI DUNIA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA
WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU. MAREHEMU BAHATI SANGA ALIKUWA
MFANYAKAZI NYUMBANI KWA DAVID KAPONDA [BABA WA WATUHUMIWA] AKIFANYA KAZI
ZA KILIMO,BIASHARA NA KUTUNZA MIFUGO. CHANZO CHA TUKIO NI UPOTEVU WA
PESA KIASI CHA TSHS 7,000,000/=.TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE
MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA INA MADHARA
MAKUBWA KATIKA JAMII NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE.
KATIKA MSAKO.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 12 KUTOKANA NA MISAKO
MBALIMBALI ILIYOFANYIKA. KATIKA TUKIO LA KWANZA JESHI LA POLISI
LINAWASHIKILIA WATU WATANO KWA KUKUTWA NA FUNGU BANDIA 203 WALIZOKUWA
WAKIZITUMIA KUFANYA UHALIFU/KUIBA KATIKA MAHOTELI MBALIMBALI JIJINI
MBEYA. WATUHUMIWA HAO NI 1. JUMA TURUKA [35], 2. BABTISTA KINUNDA [23],
3. NOEL MLELWA [20] , 4. ABDUL SALUM [36] NA 5. IDDY SADICK [26] WOTE
WAKAZI WA SOWETO JIJINI MBEYA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA YA SAA 09:00HRS ASUBUHI KATIKA
ENEO LA MABATINI JIJINI MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE
MAHAKAMANI.
KATIKA
TUKIO LA PILI JESHI LA POLISI LIMEMKAMATA JAIRO MWAKIBINGA [23] MKAZI
WA MAMA JOHN AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 250.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA YA SAA 15:30HRS ALASIRI HUKO
KATIKA MTAA WA RUANDA NZOVWE, KATA YA ILOMBA,TARAFA YA IYUNGA JIJINI
MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILIAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA
TUKIO LA TATU JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA JIJI LA
MBEYA WALIWAKAMATA WATU WANNE KWA KUFANYA BIASHARA SEHEMU ISIYORUHUSIWA.
WATUHUMIWA HAO NI 1. JOHN JACOB [25],MKAZI WA MAJENGO, 2. KHATIBU
HASSAN [31],MKAZI WA SOKOMATOLA ,3. PENDO CHAULA [29],MKAZI WA MAJENGO
NA 4. TUMAINI ERNEST [33] ,MKAZI WA ITIJI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO ENEO LA
STENDI KUU YA MABASI KATA NA TARAFA YA SISIMBA JIJINI MBEYA.
WATUHUMIWA WALIFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUPATIKANA NA HATIA, WOTE WALILIPA
FAINI YA TSHS 50,000/= KILA MMOJA.
AIDHA
KATIKA MISAKO MINGINE ILIYOFANYIKA JESHI LA POLISI LIMEFANIKIWA
KUWAKAMATA WANAWAKE WATATU 1. GRACE LUGANO [45],MKAZI WA MAFIATI, 2.
MOSHI PAUL [35] MKAZI WA IYUNGA NA 3. ELIZA DANFORD [28], MKAZI WA
NDAYELA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 4.5
PAMOJA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA NA SAA
18:00HRS JIONI HUKO KATIKA MAENEO YA MAFIATI NA IYUNGA JIJINI MBEYA.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA
DAWA ZA KULEVYA NA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA
NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII
HUSUSANI VIJANA KUKABILIANA NA UMASIKINI KWA KUFANYA KAZI HALALI BADALA
YA KUWA NA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA KWA KUFANYA KAZI HARAMU IKIWA
NI PAMOJA NA UHALIFU KWANI HATIMA WATAKUMBANA NA MKONDO WA SHERIA NA
KUKAMATWA.
Signed by:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ].
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.