CHAGUO LA GK : 'NOT FORGOTTEN' YA WATOTO CHILDREN CHOIR UGANDA
Nikiwa na Watoto Children Choir no 58 mwaka jana Big Church Day Out (BCDO) Uingereza.
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/chaguo-la-gk-not-forgotten-ya-watoto.html?m=0
![]() |
Nikiwa na Watoto Children Choir no 58 mwaka jana Big Church Day Out (BCDO) Uingereza. |
Kwaya hii ya watoto ambao wengi wao walitelekezwa na wazazi wao, wengine wakiwa yatima kutokana na vita kaskazini mwa Uganda huku wengine wakiachwa yatima kutokana na wazazi wao kufariki kwa gonjwa la ukimwi, wamekuwa wakilelewa chini ya kanisa la Watoto ambalo ibada zao huendeshwa kwa namna ya kanisa la Hillsong.
Kutoka katika kwaya hii tumekuchagulia wimbo maarufu kutoka kwao uitwao 'Not Forgotten'. Natumai utakuwa na jumapili njema kwamba licha ya yote unayopitia, kukosa wazazi, marafiki, furaha, amani lakini bado Mungu wa mbinguni hajakusahau, maana alikukomboa na anakujua kwa jina lako. Furahi sasa