Breaking News:Wabunge wa Upinzani Watoka Bungeni Baada ya CCM Kuilinda Wizara ya Nishati na Madini
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/breaking-newswabunge-wa-upinzani-watoka.html
Jioni hii
katika bunge la Bajeti Mweshimiwa Mbowe ameongoza kambi ya Upinzani
kutoka Bungeni kwa kila anachodai wabunge wa CCM wanajaribu kuficha uovu
wa Wizara ya Nishati na Madini na Kujadili mazuri tu kuhusu umeme
wakati kuna Uozo wa Kujadili ikiwemo Sakata kubwa la Ufisadi la APTL
linalohusu Wizara hiyo...
Mbowe
Amesema ni heri wao watoke na wawaachie CCM wapitishe bajeti hiyo
wenyewe kwa vile wameshapanga kuipitisha na kupanga watu wakuongea
kumsifia Waziri wa Wizara hiyo.
