BREAKIN NEWZZZ!!:- HATIMAYE MBEBEZ MUKHAREEZZZ KULIKO WOTE MBELEZZZ DMV/USA AWAFUNGA MIDOMO MAHASIDI WAKE AONYESHA BARUA ZA MUALIKO LIVE!!
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/breakin-newzzz-hatimaye-mbebez.html
Missy Temeke Mkurugenzi wa KWETU Fashions hatimaye amefunguka kutokana
na maoni ya watu waliopinga tangazo lake la kwamba amealikwa kwenye
maonyesho ya tamaduni yanayofanywa na Balozi mbalimbali Washington, DC
na kubeba jina la PASSPORT DC yakiwa chini ya Caltural Tourism DC na
yanayoadhimishwa kila mwaka wakati huu wa majira ya spring.
Missy Temeke akiongea na Vijimambo mchana leo Jumatatu May 5, 2014,
amesema wanaosema sijaalikwa sio kweli muasisi wa PASSPORT DC alinifuata
baada ya kuona meza yangu siku ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 50 ya
Muungano na kuniomba barua pepe yangu na kwamba angependa niwe mmoja ya
washiriki kwa kuiwakilisha Tanzania na pia kama naweza kuonyesha
mitindo ya mbalimbali ya nguo za KWETU Fashions. Baada ya Hapo
mawasiliano yalianza na mimi kuweka tangazo langu kwenye Vijimambo na
waosha vinywa kuanza kusukutua bila mswaki huku wengi wakidai nadanganya
na wengine kulazimisha kuleta vitu vyao bila kujua meza zimetolewa kwa
hesabu.
Mimi Barua yangu ya mwaliko hii hapa mchana kweupe na naomba aliyejileta
kwa kudai maonesho yalikuwa ya wazi naomba nae alete barua yake ya
mwaliko hapa Vijimambo.