Boko Haram kuwauza wasichana waliotekwa
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau Kundi la wapiganaji wa kislam...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/boko-haram-kuwauza-wasichana-waliotekwa.html
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau
Kundi la wapiganaji wa kislamu
nchini Nigeria la Boko Haram limesema linapanga kuwauza wasichana zaidi
ya miambili ambao liliwateka nyara wiki tatu zilizopita
Hii ni baada ya kundi hilo hatimaye kukiri
ndililo lililowateka wasichana hao baada ya kimya cha wiki tatu tangu
kutekwa nyara kwao. kuwa kundi hilo ndilo liliwateka nyara wasichana hoa.
Wasichana hao walitekwa kutoka shule moja iliyo kaskazini mashariki mwa nchi walipokuwa wajinadaa kwa mitihani yao.
Wakati huo mwanamke ambaye ni kiongozi wa maandamano nchini humo Naomi Mutah aliyekuwa amezuuiliwa na polisi kwa amri ya mke wa rais wa nchi hiyo Patience Jonathan ameachiwa huru.
Kumekuwa na shinikizo kwa serikali ya nchi hiyo kwamba haijafanya juhudi kubwa kuwaokoa wasichana hao.
Akizunguma kwa mara kwa kwaza kuhusu tukio hilpo rais wa Nigeria Goodluk Jonathan amesema kuwa atafanya awezalo kuwakoa wasichana hao.
Takriban watu 1500 wameuawa na kundi hilo mwaka huu likisema kuwa linapigana dhidi ya kile linachosema ni elimu ya kimagharabi.