BENKI YA CRDB YACHANGIA MILIONI 20 UJENZI WA KANISA LA KKKT JIMBO LA HAI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/benki-ya-crdb-yachangia-milioni-20.html
Mkurugenzi wa MasokoUtafiti, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akiwasili
katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Jimbo la Hai kwa ajili ya ibada
maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la KKKT jimbo
la Hai. Katika harambee hiyo Benki ya CRDB ilitoa shilingi milioni 20
kufanikisha ujenzi wa Kanisa na Kituo cha Watoto wanaoishi katika
mazingira magumu.
Baadhi ya waumini wakiingia kanisani
wakati wa ibada maalumu ya iliyofanyika katika Kanisa la KKKT jimbo la
Hai, iliyokwenda sambasamba na harambee ya kuchangia kanisa hilo pamoja
na Kituo cha Watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Askofu wa Jimbo la Kaskazini Dk. Martin Shao akiongoza ibada ya katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakiongozwa
na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei wakiwa katika
ibada maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Kanisa la KKKT jimbo la
hai.
Askofu wa Jimbo la Kaskazini Dk. Martin Shao akiongoza ibada ya katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipeana mkono na Askofu wa KKKT jimbo la Kaskazini, Dk. Martin Shao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
CRDB, Dk. Charle Kimei akiongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili
ya ujenzi wa Kanisa na Kituo cha Watoto wanaoisha katika mazingira
magunu
Mkurugenzi wa MasokoUtafiti, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto),
akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles
Kimei sehemu ya fedha zilizopatikana katika harambee ya kuchangisha
fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa na Kituo cha Watoto wanaoishi katika
mazingira magumu katika Kanisa la KKKT Jimbo la Hai. Hafla hiyo
ilifanyika mwishoni mwa wiki.Kulia ni Askofu wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao.