Flatnews

Balozi Seif awatahadharisha WanaCCM kujiepusha na UKAWA

Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Tanzania ameombwa kuliangalia kwa umakini kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Watanzania { UKAWA }...


Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Tanzania ameombwa kuliangalia kwa umakini kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Watanzania { UKAWA } lilioamua kuendesha mikutano ya hadhara inayoashiria mfumo wa kisiasa bila ya kuzingatia taratibu za kisheria zinazofuata usajili rasmi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubia
Ombi hilo limetolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi wakati akisalimia kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika Uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Mjini Zanzibar.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kundi hilo lililoundwa na baadhi ya Viongozi wa juu wa vyama vya Kisiasa vya Upinzani limeshindwa kutekeleza kazi waliyotumwa na Wananchi ya kutengeneza mfumo wa kupata Katiba mpya kupitia Bunge Maalum la
Katiba.
Alisema kitendo cha Viongozi hao ambacho kinawakosesha wananchi lile wanalolihitaji kinafaa kiangaliwe kwa umakini na msajili wa vyama vya siasa kwa vile kinaweza kuwakosesha wananchi hao muda wao wa kushughulikia mahitaji yao ya Kimaendeleo na kujikita zaidi katika mikutano hiyo yenye ushawishi zaidi wa kisiasa.

Balozi Seif aliwatahadharisha wana CCM na Wananchi wote kujiepusha na kundi hilo ambalo limekuwa likichukuwa kodi zao bila ya kutekeleza majukumu waliyo wakabidhi.


“ Kama kweli wana uchungu na nyinyi wananchi mbona walisubiri kwanza kutia mfukoni mkwanja { posho } halafu ndio wakaingia mitini kuvikimbia vikao vya Bunge Maalum kwa kujenga hoja “. Alisema Balozi Seif.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM aliwaonya wale viongozi wa siasa wenye tabia ya kumsakama katika majukwaa ya kisiasa kuachana na tabia hiyo mara moja kwa vile wengi kati yao anawaelewa udhaifu wao wa Kisiasa.

Alisema endapo kama viongozi hao wataendelea na hulka hiyo waelewe kwamba muda si mrefu atalazimika kufichua maovu na aibu zao.

Post a Comment

emo-but-icon

item