ANGALIA PICHA MWANAMKE ALIYECHEZEWA MCHEZO NA KUOLEWA ILI APATE UKIMWI, DAKTATI AHUSIKA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/angalia-picha-mwanamke-aliyechezewa.html
Na Chande Abdallah
UKISIKIA
simulizi ya Hafsa Ramadhani (19) itakutia simanzi, itakutesa moyo na
kukutoa machozi, huwezi kuamini aliingia kwenye ndoa bila kujua kuwa
alikuwa akienda kukutana na
ugonjwa wa ukimwi, Risasi Mchanganyiko linakufunulia.
Habari
kutoka chanzo chetu cha kuaminika zinasema, binti huyo alifanyiwa
mipango ya ndoa bila yeye na mumewe huyo kupima kwanza maambukizi ya
ugonjwa huo, ingawa tahadhari hiyo ilitolewa mapema kwa kuwa muoaji
alikuwa akijulikana kuwa aliishi na ugonjwa huo kwa muda mrefu.
ILIKUWAJE?
“Huyo
binti alitokea Bukoba, akaja hapa Dar es Salaam kutafuta kazi. Akaanza
kufanya kazi za ndani, akiwa mdogo kabisa. Alihangaika kwenye nyumba
mbalimbali lakini baadaye akafikia kwenye kituo cha watoto yatima (kwa
sasa tunahifadhi jina), kipo Charambe ambapo alianza kuishi hapo,”
kilipasha chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
“Alipofikisha
umri wa miaka 15 tu, wale watu wa pale kituoni wakamuozesha kwa jamaa
mmoja (jina tunalo) ambaye kwa sasa ni marehemu. Huyo jamaa alikuwa
akiishi na VVU na mbaya zaidi, hao watu wa hapo kituoni, walishauriwa
kuhusu jambo hilo wakapuuza, ndiyo maana wengi wanaamini walimfanyia
makusudi,” kilieleza chanzo hicho ambacho kimedai kipo karibu na binti
huyo.
HUYU HAPA HAFSA
Timu ya gazeti hili kwa msaada wa chanzo chetu, ilifanikiwa kukutana
na Hafsa ambaye kwa mwonekano ni binti mdogo na mpole kiasili,
akazungumza mengi yanayomsibu katika maisha yake.
“Sikujua kama maisha yangu yangeishia hivi. Sikutegemea kama
ningeteseka kiasi hiki. Kwanza mimi sijawahi kuwaona wazazi wangu.
Niliambiwa tu walikufa tangu nikiwa mdogo, kwa hiyo nilikulia kwa wazazi
wa kufikia huko Bukoba,” anaanza kusimulia Hafsa.
Akaendelea: “Baada ya kuolewa, maisha yalikuwa ya shida sana.
Nilichukuliwa hapa Dar na kwenda kuishi na huyo mume wangu Arusha baada
ya kufunga naye ndoa. Alikuwa haniachii fedha ya matumizi wakati
mwingine lakini hali yake ya kuugua kila mara iliniogopesha ingawa
sikuwahi kufikiria kabisa suala la ukimwi.
“Nilibahatika kupata mtoto na huyo bwana na hapo ukawa mwanzo wa mimi
kuanza kuugua mfululizo. Nikiwa bado naumwa, mume wangu alifariki
dunia. Basi, maisha yangu yakazidi kuwa magumu maana sikuwa na msaada
wowote.”
DOKTA AMWAMBIA UKWELI
“Nikiwa nakwenda kliniki huku afya yangu ikiwa si ya kuridhisha,
daktari mmoja alinishauri nifanyiwe vipimo. Ilibidi nishauriwe sana
kabla ya kupimwa na kwa bahati mbaya nikagundulika kuwa nina ukimwi.
Hata mwanangu pia ameathirika.
“Najua walinificha kwa muda mrefu kutokana na umri wangu, maana sasa
nina miaka 19 na mwanangu mitatu, kwa hiyo wakati najifungua nilikuwa na
16 tu. Naiona dunia chungu kwa kweli.”
MAISHA MAGUMU ARUSHA, ARUDI DAR
“Kutokana na maisha ya mateso ya ndugu wa mume wangu kule Arusha,
nilijikusanya nikapata nauli, nikaamua kutoroka na kurudi zangu Dar.
Sikuwa na mahali pengine pa kwenda zaidi ya kurudi kituoni nilipokuwa
nalelewa.”
ANYANG’ANYWA MWANAYE
“Mwanangu ndiye alikuwa faraja yangu pekee lakini wakwe zangu
walikuja kuninyang’anya mtoto wakisema eti sina uwezo wa kumlea. Kwa
kuwa ni damu yao, sikuwa na jinsi ikabidi nikubali tu. Sasa hivi anaishi
nao huko Temeke.
“Nashukuru Mungu, nilipata msamaria (aliomba asitajwe jina lake)
ambaye aliguswa na ugumu wa maisha yangu, akanikaribisha nyumbani kwake.
Naishi naye Mbagala – Zakheem (Dar), lakini nina ugumu wa maisha. Kama
unavyojua, siwezi kumtegemea yeye kwa kila kitu.”
ANAHITAJI MSAADA WAKO
Kama umeguswa na kisa cha Hafsa na ungependa kumsaidia kwa hali na
mali, unaweza kufanya hivyo kwa kutumia namba 0783 855453 au 0713522779.