ANGALIA PICHA MAAJABU YA MUNGU!
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/angalia-picha-maajabu-ya-mungu.html
Paul Ngido na Asha Yahya wanaolelewa kwenye kituo cha watoto wenye matatizo mbalimbali waliowazaa watoto Keisha na Glory.
KATIKA
hali ya kushangaza, wagonjwa wa mtindio wa ubongo, Paul Ngido na Asha
Yahya wanaolelewa kwenye kituo cha watoto wenye matatizo mbalimbali
wakiwemo yatima cha Ngido kilichopo Mazimbu FK mkoani hapa wamejikuta
wakizaa watoto wawili, Keisha na Glory ndani ya kituo hicho.Mkurugenzi
mkuu wa kituo hicho, Linda Cyprian Ngido amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo kwenye kituo chake na kusema kwamba huo nao ni msalaba
anaotakiwa kuubeba.
Uwazi lilimuuliza mkurugenzi huyo kwa nini wazazi hao wasiruhusiwe kubariki ndoa na kuishi kama mume na mke, alijibu:
Paul
Ngido na Asha Yahya wanaodaiwa kuwa na mtindio wa ubungo wakiwa na
watoto wao wawili waliozaa ndani ya kituo hicho, Keisha na Glory.
“Niliwahi
kuongea na mchungaji kuhusu hilo, lakini akakataa akidai hawezi
kufungisha ndoa ya watu wenye upungufu wa akili.“Kama wewe (mwandishi)
utanisaidia kufanikisha jambo hilo nitashukuru sana,” alisema mkurugenzi
huyo.
Baada
ya majibu hayo mwandishi wetu alikwenda kwenye Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania ‘KKKT’ Dayosisi ya Morogoro na kuonana na Askofu
Jacon Mameo. Aliulizwa kuhusu wazazi hao, akasema:
“Kwanza
taarifa hizo nzito ndiyo nazisikia kwako. Huyo mchungaji alifanya
makosa, neno ndoa ni muungano wa watu wawili, mwanamke na mwanaume hivyo
kama watu wameungana na kufanikiwa kuzaa watoto na kuwalea vizuri hao
wana akili timamu, tena wako kwenye uangalizi wa kituo, labda
kipingamizi kiwe kwa wazazi kwani ndoa haiwezi kufungwa kama wao
hawajakubali,” alisema askofu huyo.
Mwandishi
wetu alirudi tena kweye kituo hicho na kuzungumza na familia hiyo. Wa
kwanza alikuwa Paul ambapo alisema: “Mimi wazazi wangu siwajui, mama
yangu ni huyu (mkurugenzi wa kituo) na ndiyo maana amenipa majina
mapya”.
Kwa upande wake, Asha
alipoulizwa kama wazazi wake wameridhia kubadili dini na kufunga ndoa
ya Kikristo na Paul alisema: “Ndiyo.”
Mwandishi wa habari hii
atabeba jukumu la kutoa sehemu ya mahari hiyo ili wawili hao wafunge
ndoa lakini mpaka pale wataalam watakapothibitisha kwamba sasa wazazi
hao wako fiti kiakili (anafuatilia).
Kituo hicho kina watoto na
watu wazima 53 wenye matataizo ya mtindio wa ubongo, watoto 10 waliokuwa
wakiishi katika mazingira magumu, baadhi yao wakiwa yatima.