WAZIRI MKUU WA KOREA KUSINI AJIUZURU: NI BAADA YA AZOMEWA ALIPOTEMBELEA FAMILIA ZA WAATHIRIWA WALIOTOWEKA KATIKA FERRY BAADA YA KUZAMA KATIKA HALI YA KUTATANISHA.
https://samchardtz.blogspot.com/2014/04/waziri-mkuu-wa-korea-kusini-ajiuzuru-ni_28.html
Waziri
mkuu nchini Korea Kusini amejiuzulu kutokana na vile serikali yake
ilivyolichukulia swala lote la ferry iliozama siku kumi na moja
zilizopita.Chung Hong Won amesema kuwa kusalia afisini ni mzigo mkubwa kwake.Bwana
Chung alizomewa alipozitembelea familia za waathiriwa waliotoweka
katika ferry hiyo ya Sewol,baada ya kuzama katika hali ya kutatanisha.

Takriban
watu 200 wanadaiwa kufa maji katika tukio hilo huku zaidi ya mamia
wengine wakiwa hawajulikani waliko,wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu
waliokuwa wakielekea katika ziara ya shule.
Wapiga mbizi bado wanaendelea kuwasaka waathiriwa chini ya ferry hiyo iliozama.
Ripoti za awali zimedai kuwa watu wote wametolewa katika boti hiyo.
CHANZO BBC
