Flatnews

MKURUGENZI WA VHM ANUSURIKA NA MAJAMBAZI ASUBUHI YA LEO

Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa huduma ya sauti ya matumaini (VHM).


Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa huduma ya sauti ya matumaini (VHM).

Ikiwa takribani siku tano tangu kundi la wainjilisti wa huduma ya sauti ya matumaini (VHM) kuvamiwa na watu wasiojulikana na kuporwa pesa pamoja na vitu vingine wakiwa njiani kuelekea mkoani Mororgoro kwa injili , usiku wa kuamkia leo mkurugenzi wa huduma hiyo mchungaji Peter Mitimingi amenusurika mikononi mwa majambazi akiwa anatoka nyumbani kwake kuelekea katika shughuli zake za kila siku.

Ufuatao ni ushuhuda wa mchungaji Mitimingi akieleza juu yaa tukio zima lilivyokuwa asubuhi ya leo kama alivyoandika kupitia ukurasa wake wa facebook "Niliondoka kwangu saa 10.30 alfajiri ya leo nikapita katika mtaa mmoja jirani na mitaa ya home kuna kama kapori fulani nikaona gari ndogo aina ya RAV4 imepaki pembeni ikiwa imezimwa nilipoanza kuisogelea ikawashwa na mara ikaanza kutembea ikiwa mbele yangu. Taa nyekundu moyoni zikawaka nikatilia mashaka nikapunguza mwendo nikaamua kui-overtake mara ikawa inatembea katikati ya barabara kunizuia nisi-overtake mara ikasimama barabarani katikati nikaona mlangoo mmoja wa nyuma ukifunguuka, yaani nadhani malaika walishuka wakakalia usukani maana ilikuwa ni kitendo cha sekunde kadhaa niligeuza gari na kurudi nilikokuwa nimetokea kwa speed isiyo ya kawaida. nikaiaaccha iile gari imesimama barabarani katikati wasijuee cha kufaanya baada ya hapo". Amesimulia mchungaji Mitimingi.

Post a Comment

emo-but-icon

item