ANGALIA PICHA MTOTO ALIYEAJIRIWA ADAI KUTESWA NA KUPOKEA KIPIGO KUTOKA KWA BOSI WAKE
https://samchardtz.blogspot.com/2014/04/angalia-picha-mtoto-aliyeajiriwa-adai.html
Mtoto
mwenye umri wa miaka (14) ambaye ni mwenyeji wa Rombo mkoani
Kilimanjaro anayeripoti manyanyaso kutoka kwa mtu anayedaiwa kuwa bosi
wake.
Mtoto mwenye umri wa miaka (14) anadaiwa kuajiriwa akiwa na umri mdogo kinyume cha sheria za kazi kisha kupokea kipigo na manyanyaso kutoka kwa mtu anayedai ni bosi wake aliyemtaja kwa jina moja la Agness.
Kwa mujibu wa mashuhuda, mbali na kuwepo kwa malalamiko ya unynyasaji
juu ya mtoto huyo, siku ya tukio mwajiri wake alimpa kipigo kwa madai
kwamba alimuibia shilingi laki saba dukani alikomwajiri maeneo ya
Mwananyamala, Dar hivi karibuni.
Mtoto
huyo ambaye ni mwenyeji wa Rombo mkoani Kilimanjaro alizama jijini Dar
na kuajiriwa katika duka hilo mwanzoni mwa mwezi Novemba, mwajka jana.
Akizungumza
na mwanahabari wetu kwa masikitiko, mtoto huyo alisema tangu aajiriwe
na mama huyo hajawahi kulala nyumbani bali alikuwa akilala hukohuko
kwenye duka ambalo ni dogo halafu limejaa vitu vingi na alikuwa
akifungua saa 12:00 asubuhi na kufunga saa 5:00 usiku kila siku.
Alidai
kuwa hajawahi kulipwa mshahara ambao walikubaliana kwa malipo ya
shilingi 25,000/= ambazo bosi huyo alitakiwa kuzituma kwa mama mzazi wa
mtoto aliyeko Rombo.
Akielezea kwa uchungu mateso aliyoyapata tangu afike kwa mama huyo,
mtoto alidai alikuwa akipigwa bila sababu na kusingiziwa kuwa ameiba
fedha kisha kunyimwa chakula.
Kwa
mujibu wa mtoto huyo, kuna mama mmoja jirani yao aliyekuwa akishuhudia
mateso yake hivyo akawatafuta wanaharakati wa haki za binadamu ambao
walichunguza ishu na wakajiridhisha kweli mtoto huyo alikuwa
akinyanyaswa. Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wanaharakati hao
alisema kwa kuwa walishatoa elimu mitaani na kama yakitokea masuala kama
hayo basi wananchi wawasiliane nao.
Mwanaharakati
huyo alisema kuwa walipigiwa simu wiki mbili zilizopita kuwa kuna mtoto
anateswa ndipo walipofanya uchunguzi katika eneo alilokuwa akifanyia
kazi.
Wanaharakati
hao waliwasiliana na polisi wa Kituo cha Oysterbay, Kinondoni, Dar
ambapo mama huyo alikamatwa na kufunguliwa jalada la kesi namba
OB/RB/5205/2014 UNYANYASAJI WA MTOTO huku akisubiri kufikishwa kwa
kortini.
