YAYA TOURE APANDISHWA JUU NI KATIKA HARAKATI ZA KUSAKA GOLI
Moja ya viungo wanaotegemewa na Manchester City ni Yaya Toure na uwepo wake uwanjani huifanya timu icheze kwa usalama zaidi, lakini k...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/yaya-toure-apandishwa-juu-ni-katika.html
Moja
ya viungo wanaotegemewa na Manchester City ni Yaya Toure na uwepo wake
uwanjani huifanya timu icheze kwa usalama zaidi, lakini kuna stori mbaya
kuhusu mchezaji bora huyu wa Afrika.
Yaya
Toure amepandishwa ndege ‘Mwewe’ kurudi England kwa matibabu zaidi
baada ya kuumia katika mechi ya kirafiki iliyopigwa jana , Melbourne,
Australia dhidi ya miamba ya kandanda ya Hispania, Real Madrid.

Toure
aligongana na golikipa wa Madrid, Keylor Navas ambaye alitoka kwenda
kupiga ngumi mpira na Muivory Coast huyo akagongana naye.
Klabu
yake imeamua kumrejesha England ili kumtibu kwa umakini, hivyo atakosa
mechi za maandalizi ya msimu zitakazopigwa huko Vietnam.

Wakati
huo huo, Delph naye alipata majeraha ya nyama za paja katika mechi ya
kwanza akiichezea Man City na kutolewa nje kwa machela dakika 20 tu
baada ya mechi na inabidi atibiwe haraka kabla ya kuanza msimu mpya.
