PICHA 8 CHELSEA WAKIFUMULIWA MAREKANI…
Eden Hazard akionesha mambo yake Mabingwa wa kandanda England, Chelsea wameanza vibaya ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya nchini ...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/picha-8-chelsea-wakifumuliwa-marekani.html
Eden Hazard akionesha mambo yake
Mabingwa wa kandanda England,
Chelsea wameanza vibaya ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya nchini
Marekani baada ya kupokea kipigo kikali cha 4-2kutoka kwa New York Red
Bulls.
Mabao ya Chelsea yamefungwa Loic Remy (26) na Eden Hazard (75).

Waliocheka na nyavu kwa upande wa Red Bulls ni Franklin Castellanos (51), Tyler Adams (67) na Sean Davis (73, 78).
Hata hivyo Jose Mourinho
amesema kikosi chake kimefanya mazoezi kwa wiki moja tu, hivyo wachezaji
hawana kasi kwasababu wamechoka.

Straika wa Chelsea, Diego Costa akijaribu kumfunga Golikipa Santiago Castano

Mlinzi wa Chelsea, Branislav Ivanovic, akichuana na mchezaji wa New York Red Bulls

Kiungo wa Chelsea, Ramires akipambana na kiungo wa New York Red Bulls, Davis

Victor Moses, ambaye amerejea kutokea Stoke ambako alikuwa anacheza kwa mkopo akimtoka Daniel Bedoya

Oscar akijaribu kumiliki gozi

