Obama, Kenyatta kuwajadili Al shabaab
Rais wa Marekani Barack Obama akiwa na bibi yake Mama Sarah Obama kushoto na dada yake Auma Obama katika chakula cha jioni na wanandug...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/obama-kenyatta-kuwajadili-al-shabaab.html

Rais
wa Marekani Barack Obama akiwa na bibi yake Mama Sarah Obama kushoto na
dada yake Auma Obama katika chakula cha jioni na wanandugu wa familia
ya Obama nchini Kenya.
Rais wa Marekani Barack Obama aliyewasili nchini Kenya anatarajia kukutana na Rais Uhuru Kenyatta kwa mazungumzo ambapo wataangazia usalama wa kanda hiyo na tisho kutoka kwa kundi la kigaidi la Al shabaab.
Miongoni mwa mambo mengine atakayoa angazia ni kuhutubia kongamano la wajasiriamali pamoja na masuala ya ufisadi ulioitikisa nchi hiyo na kupelekea vigogo kadhaa kusimamishwa kazi.
Rais Obama baadaye atatembelea eneo kulikotokea shambulizi la kigaidi katika uliokuwa ubalozi wa marekani mjini Nairobi na pia kukutana na rais wa kenya uhuru.
Nchi ya Marekani imekuwa ikiisadia kenya katika vita dhidi ya ugaidi na imewaua vongozi kadha wa kundi la al shabaab kwenye mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani.