KOCHA WA MAN U VAN GAAL AMTAMKIA HAYA DAVID DE GEA……
Louis Van Gaal amemwambia golikipa wake, David De Gea kwamba anataka acheze dhidi ya Barcelona katika mechi ya kirafiki itakayochezwa...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/kocha-wa-man-u-van-gaal-amtamkia-haya.html
Louis
Van Gaal amemwambia golikipa wake, David De Gea kwamba anataka acheze
dhidi ya Barcelona katika mechi ya kirafiki itakayochezwa kesho Jumamosi
nchini Marekani ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa Premier League.
Matatizo
ya mgongo yalimuweka nje ya uwanja, De Gea katika mechi mbili za
Manchester United nchini Marekani, lakini Van Gaal baada ya kumpeleka
Hospitali mjini California kufanyiwa uchunguzu, imeonekana hana tatizo.

Wakati
msimu mpya unakaribia kuanza, De Gea ameonesha kutaka kuondoka Old
Trafford kwenda Real Madrid, lakini Meneja wa Man United imesema
anatakiwa ku-focus kuitumikia klabu yake ya sasa.
Jumanne
ya wiki hii, De Gea aliombwa kuungana na wenzake kwenye ‘warm-up dhidi
ya San Jose Earthquakes, lakini hakufanya lolote, ila sasa Van Gaal
anatumaini kwamba atacheza dhidi ya Barcelona mjini Santa Clara.
Van
Gaal amesema: “Nina matumaini kwamba anaweza kucheza dhidi ya Barcelona.
Alipata majeruhi (mapema wiki hii), nimemwambia akasimame golini
kuwaongoza washambuliaji wangu, lakini asifanye chochote kinachoweza
kumpa madhara” Amesema Van Gaal.
