Joshua Nasssari Achaguliwa tena Kupeperusha Bendela ya CHADEMA Jimbo la Arumeru Mashariki
Aliekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha,Joshua Nassari akizungumza namna alivyotekeleza ahadi zake katika kipindi ...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/joshua-nasssari-achaguliwa-tena.html

Aliekuwa
Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha,Joshua Nassari akizungumza
namna alivyotekeleza ahadi zake katika kipindi kilichopita wakati wa
mkutano Mkuu wa Jimbo uliofanyika kwenye Mji mdogo wa Usa River ambapo
alichaguliwa bila kupingwa ili kupeperusha bendera ya Chadema katika
uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Wanachama
wa Chadema wakipiga kura za maoni kwaajili ya kumchagua mgombea ubunge
jimbo la Arumeru Mashariki katika Mji Mdogo wa Usa River,Joshua Nassari
alipata kura 387 na kura 2 za hapana.

Wanachama wa Chadema wakifurahia jambo katika mkutano huo

Mwenyekiti
wa Kanda ya Kaskazini ambaye alikua Mbunge wa Chadema jimbo la Karatu
mkoa wa Arusha,Israel Natse(kulia)na Katibu wa Chadema mkoa wa
Arusha,Kalist Lazaro wakimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru
Mashariki, Joshua Nassari(kati)baada ya kutangazwa mshindi.