HUU NDIO UGUMU WA KIPUTE CHA YANGA vs KMKM LEO….
MABINGWA wa kandanda Tanzania bara, Young Africans leo wanahitaji ushindi mzuri dhidi ya KMKM ya Zanzibar ili kujihakikishia kucheza ...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/huu-ndio-ugumu-wa-kipute-cha-yanga-vs.html
MABINGWA wa kandanda Tanzania
bara, Young Africans leo wanahitaji ushindi mzuri dhidi ya KMKM ya
Zanzibar ili kujihakikishia kucheza hatua ya Robo Fainali ya Kombe la
Kagame linaloendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaam.
Wakati huo huo, KMKM nao wanahitaji ushindi ili kujihakikishia kwenda Robo Fainali.
KMKM na Yanga SC zote zina
pointi tatu baada ya kila timu kushinda mechi moja hadi sasa, dhidi ya
wapinzani mmoja, Telecom ya Djbout.
KMKM walishapoteza mechi mbili
baada ya kufungwa 2-1 na Khartoum N na 3-1 dhidi ya Gor Mahia, wakati
Yanga SC imepoteza mechi moja tu dhidi ya mabingwa mara tano wa michuano
hiyo Gor Mahia.

Kikosi cha timu ya KMKM ya Zanzibar kinachopambana na Khartoum National Club ya Sudan
Endapo KMKM itafungwa leo, watatupa nje ya michuano hiyo.
Yanga SC ikicheza leo itabakiwa
na kibarua kigumu dhidi ya vinara wa kundi A, Khartoum National Club
ya Sudan ambayo itakuwa ya mwisho baada ya kucheza na KMKM .
Khartoum ina pointi sita, mabao
saba ya kufunga na moja la kufungwa, wakati Gor Mahia walio nafasi ya
pili wana ponti sita, mabao matano ya kufunga na mawili ya kufungwa.
Yanga SC inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu, mabao manne ya kufunga na mawili ya kufungwa, wakati KMKM ina pointi tatu, mabao matatu ya kufunga na matano ya kufungwa.
Telecom ya Djibouti ambayo itacheza mechi ya mwisho na Gor Mahia kabla ya kurejea kwao imepoteza mechi zote tatu.
Ilifungwa 1-0 na KMKM, ikafungwa 5-0 na Khartoum na jana imefungwa 3-0 na Yanga SC.

Timu tatu kati ya tano za kundi
hilo zitakwenda Robo Fainali kuungana na washindi wawili wa kila kundi B
na C pamoja na mshindi wa tatu bora kutoka makundi hayo.