Flatnews

Burundi: Upinzani wapendekeza serikali ya muungano

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Ikiwa matokeo ya uchaguzi wa urais yakitarajiwa kutangazwa wiki hii, kiongozi wa upinzani n...


Burundi Präsident Pierre Nkurunziza Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza


Ikiwa matokeo ya uchaguzi wa urais yakitarajiwa kutangazwa wiki hii, kiongozi wa upinzani nchini humo amemtolea wito rais Pierre Nkurunziza kukubali pendekezo la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Wito huo umetolewa na kiongozi wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa ambaye amemtaka rais Pierre Nkurunziza, kuitisha mazungumzo na wapinzani na kuunda serikali ya muungano wa kitaifa kufuatia uchaguzi wenye utata. Rwasa amesema pendekezo lake hilo, linaweza kusaidia kurejesha amani nchini humo.
Rwasa ambaye kama rais Nkurunziza aliwahi kuwa muasi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi ameliambia shirika la habari la Reuters, kwamba kuna ulazima wa hatua za haraka kuchukuliwa hivi sasa, ili kuwazuwia magenerali waliopanga jaribio la mapinduzi la Mei, kuzusha tena vurugu wakati ambapo tayari nchini hiyo imo katika mzozo wa kisiasa. Mzozo huwo uliosababishwa na uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza, kugombea muhula wa tatu madarakani.
Upinzani unamlaumu rais Nkurunziza kukiuka katiba kwa kugombea muhula wa tatu madarakani, na hivyo ulisusia uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne iliyopita (21.07.2015) jambo ambalo linampa nafasi kubwa Nkurunziza kuibuka na ushindi. Rais Pierre Nkurunziza kwa upande wake amekanusha kuvunja sheria yoyote, akisema sheria ya mahakama inamruhuusu kugombea tena urais kwa mara ya tatu. Matokeo ya uchaguzi huwo, yanatarajiwa kutangazwa wiki hii.
Agathon Rwasa früherer Rebellenführer in Burundi Präsidentenwahl 2015 Kandidatur Kandidat Kiongozi wa upunzani Burundi, Agathon Rwasa
Nkurunziza akubali pendekezo
Mshauri wa rais Nkurunziza Willy Nyamitwe amesema rais Nkurunziza hatopinga pendekezo la serikali ya umoja wa kitaifa, na kuongeza kuwa serikali iko tayari kwa hilo lakini haitokubali kufanya hivyo kwa masharti yoyote.
Rwasa, kiongozi wa umoja wa upinzani wa Amizero y'Abarundi, aliliambia shirika la habari la Reuters, kwamba kuna baadhi ya wapinzani ambao tayari wameshatishia mapigano ya kutumia silaha.
Halikadhalika moja ya majenerali waliohusika na jaribio la mapinduzi ya Mei, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa matumizi ya nguvu ndio njia pekee iliyosalia ya kumuondoa rais Nkurunziza, baada ya njia za mazungumzo na shinikizo la kimataifa, kushindwa kumzuia kugombea muhula wa tatu madarakani.
Mgogoro huu wa sasa ambao ni mbaya zaidi tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2005 umeleta mvutano mkubwa katika nchini Burundi ambayo iko katika aneo lenye historia ya vita vya kikabila.
Rwasa amesisitiza kuwa kwa masilahi ya Warundi, serikali ya muungano wa kitaifa ni suluhisho litakaloweza kukubalika.

Related

NEWS 3712494199919790453

Post a Comment

emo-but-icon

item