ARSENAL MLIE TU KWA BENZEMA
Benzema wa Real Madrid Hatimaye wakala wa mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema amethibitisha kuwa uwezekano wa nyota huyo kuih...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/07/arsenal-mlie-tu-kwa-benzema.html
Benzema wa Real Madrid
Hatimaye wakala wa mshambuliaji
wa Real Madrid, Karim Benzema amethibitisha kuwa uwezekano wa nyota huyo
kuihama klabu yake ya Real Madrid na kujiunga na Arsenal ni jambo la
kuchekesha.
Wakala huyo amethibitisha kuwa ana zaidi ya 1000% kwamba Benzema atabakia klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi.
Taarifa hizo zimekuja kama mkuki
ndani ya moyo wa mashabiki wa Gunners ambao wiki hii yote walikua na
matumaini ya kumpata nyota huyo.
Nyota huyo wa zamani wa klabu ya
Olympic Lyon ya Ufaransa, amekuwa katika headlines kwa muda sasa tangu
kuwasili kwa kocha Rafa Benitez kikosini hapo, ambapo tetesi zimekuwa
zikidai huwenda Cristiano Ronaldo akacheza nafasi ya Karim Benzema,
ushambuliaji wa katikati.
Mshambuliaji huyo ambaye ni
mfaransa amekuwa akihusishwa sana na kutua Emirates, lakini kauli hizi
za agent wake zinazima ndoto za kocha Arsene Wenger pamoja na mashabiki
kwa ujumla.
Klabu ya Arsenal imekuwa
ikikosolewa mara kwa mara kutokana na kukosa mtu mwenye uwezo wa kufunga
na kuwatesa mabeki wa timu pinzani na sasa wanahaha kutafuta mtu.
Aidha legendari wa klabu hiyo ya
Arsenal, Thierry Henry amekua haridhishwi na uwezo wa mshambuliaji wa
sasa wa gunners, Oliver Giroud.
