Faiza Ally akata rufaa, ataka kurudishiwa mtoto wake
Siku chache zimepita tangu Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kushinda kesi na kumchukua mtoto wake Sasha, aliyezaa ...
http://samchardtz.blogspot.com/2015/06/faiza-ally-akata-rufaa-ataka.html

Siku chache zimepita tangu Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kushinda kesi na kumchukua mtoto wake Sasha, aliyezaa na mwanadada Faiza Ally, kwa madai kuwa mzazi mwenzake huyo ameshindwa kumlea kutokana na kukosa maadili, hatua hiyo imepelekea Faiza kukata rufaa ya kutaka arudishiwe mtoto wake.
Kupitia mtandao wa kijamii amesema kuwa “Nasitikishwa sana na maneno
yenu makali hasa nyinyi mnao sambaza kashfa juu yangu kuhusu mavazi
yangu- hakuna hiyo sheria tanzania inayosema nipokonywe mtoto kuhusu
mavazi yangu”.
“Nimekata rufaa na nawahakikishia nitashinda kesi na nitamlea
mwanangu na nitavaa mavazi yangu na nita enjoy maisha yangu/ nina
mwanasheria makini aliesomea sheria na sisi nyinyi mnao nipa hukumu humu
ndani na kwingine! pamoja na mavazi yangu mimi ni mama bora!”
“Mnajua upande wangu lkn hamjui upande wa sugu na hakika mengi
mtayajua kupitia kesi hii/ mavazi yangu nayapenda na kwa mujibu wa
sheria si kitu kinacho nifanye ni pokonye mtoto wangu-maneno yenu
machafu dhidi yangu yananiuma sana lakini kamwe hayata nirudisha nyuma
katika kutetea haki yangu!”.
“Namjua sugu na na ninajiua mm ktk ubora wangu katika malezi ya
mwanangu/ mm ni mama na si mama tu ni mama bora kwa sasha na ananihitaji
na sitamuacha na nyinyi wajinga wachache endeleeni kuniponda na kuona
na stahili kupata pigo hili na si wote”.
“Kuna wengine wema kwa upande wangu na washukuru na nina waahidi
sitawarudisha nyuma nitasimama mpaka kieleweke- sasa hivi ni jasiri
kupita maelezo ��…..in god we trust inshaallah…”.