Kiongozi wa upinzani auawa Urusi
Maafisa wa polisi wakiweka usalama katika eneo ambalo kiongozi wa upinzani nchini Urusi Boris Nemtsov aliuawa
http://samchardtz.blogspot.com/2015/02/kiongozi-wa-upinzani-auawa-urusi.html
Maafisa wa polisi wakiweka usalama katika eneo ambalo kiongozi wa upinzani nchini Urusi Boris Nemtsov aliuawa
Mmoja wa wanasiasa maarufu wa upinzani nchini Urusi Boris Nemtsov
ameuawa kwa kupigwa risasi kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Moscow.
Mwanasiasa
huyo alipigwa risasi nne kutoka nyuma na watu waliokuwa ndani ya gari
alipokuwa akitembea nje ya makao makuu ya serikali.Bwana Nemtsov ambaye alihudumu kama naibu waziri mkuu wakati wa uongozi wa rais Boris Yeltsin alikuwa akimshutumu vikali rais Vladimir Putin.
Boris Nemtsov
Alikuwa akipanga mkutano ambao ungefanyika kesho Jumapili kupinga kile alichokitaja kuwa vita vinavyoendeshwa na Urusi nchini Ukrain.
Kwenye mahojiano mapema mwezi huu bwana Nemtsov alisema kuwa alikuwa na hofu kuwa rais Putin angemuua.
