TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI DAR KUTATULIWA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/tatizo-la-msongamano-wa-magari-dar.html
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(kulia),akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam kuhusu ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa
7.5 litakaloanzia eneo la Aghakani na kuishia Coco beach, ujenzi huo
unaotarajiwa kuanza mapema mwakani na unafadhiliwa na Serikali ya watu
wa Korea Kusini ,lengo ni kupunguza msongamano wa magari katika daraja
la Serender,kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt. Juma Iyombe.
(Picha Lorietha Laurence –Maelezo)
………………………………………………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo -Maelezo
Zaidi
ya Bilioni 110 zinatarajia kutumika katika ujenzi wa daraja lenye urefu
wa kilometa 7.5 ili kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Magufuli alisema daraja hilo litaanzia eneo la Aghakani na kuishia
Coco beach.
Waziri
Dkt. Magufuli alisema daraja hilo litakalojengwa kwa msaada wa
Serikali ya Korea Kusini litakuwa na njia nne na barabara mbili za
huduma kwa kila upande lenye uwezo wa kupitisha magari elfu 61 kwa siku
.
“Serikali
ya Korea Kusini imemaliza mradi wa ujenzi wa daraja la Kikwete pamoja
na barabara ya Malagalasi Mkoani Kigoma na sasa tumewaomba waendelee
kutoa msaada kwa ajili ya ujenzi wa barabara mkoani Dar es Salaama ili
kupunguza msongamano wa magari”, alisema Dkt. Magufuli.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu kutoka TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale
amebainisha kuwa wataalamu kutoka Korea Kusini wameshafanya Upembuzi
yakinifu uliomalizika hivi karibuni, hivyo ujenzi wa daraja hilo
unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwaka ujao.
Aliongeza
kuwa daraja hilo litakalofahamika kwa jina la New Salender Bridge
litaunganishwa na barabara ya Ally Hassan Mwinyi kutokea Aghakani na kwa
upande mwingine litaunganishwa na barabara ya Chole iliyopo Masaki.
Serikali
imeweka mikakati mingi ya kupunguza msongamano wa foleni za magari kwa
kuanzisha ujenzi mbadala wa barabara za juu unaotarajiwa kujengwa maeneo
ya TAZARA,Mbagala rangi tatu hadi gerezani, kuanzishwa kwa kivuko cha
Dar es Salaam hadi Bagamoyo.
Pia
utafanyika utanuzi wa barabara nyingine za Dar es salaam kwenda
Morogoro kupitia Chalinze na ile ya Morocco hadi Mwenge na Bagamoyo
hadi Msata.