MSANII WA BONGO MOVI, MAYA APIGWA MAOMBI KISA MITUNGI
MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amezuiwa kunywa pombe baada ya kuangushiwa maombi mazito na kushauriwa kubadil...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/msanii-wa-bongo-movi-maya-apigwa-maombi.html
MUIGIZAJI wa
sinema za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amezuiwa kunywa pombe baada ya
kuangushiwa maombi mazito na kushauriwa kubadilika kitabia.
Chanzo
makini kimepenyeza habari kuwa, juzikati Maya alifika katika kanisa
moja lililopo Mbezi jijini Dar na kuombewa kisha mchungaji wa kanisa
hilo akamzuia kunywa pombe.
“Kazuiwa lakini najua kwake itakuwa mtihani, sidhani kama ataacha kweli,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa Maya, alikiri kuombewa lakini alipotajiwa suala la kuzuiwa pombe na kama ataweza kweli kuacha, alikata simu ghafla.
