Lulu asema hana muda wa kupoteza kwa mwanaume!
Msanii wa filamu Elizabeth Michael a.k.a Lulu amesema kuwa kwenye maisha yake kwa sasa hatakuwa na muda wa kupoteza kwenye mapen...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/lulu-asema-hana-muda-wa-kupoteza-kwa.html
Msanii
wa filamu Elizabeth Michael a.k.a Lulu amesema kuwa kwenye maisha yake
kwa sasa hatakuwa na muda wa kupoteza kwenye mapenzi bali anaelekeza
nguvu zake katika kazi.

Akizungumza
na Mwanaspoti hivi karibuni, nyota huyo wa filamu za kibongo alisema ni
bora atumie muda huu kutafuta maisha ili watoto wake waje kuishi
vizuri.
“Kuliko
kupoteza muda na nguvu kwa mwanaume, bora nijitunze kwa ajili ya
kuwalea wanangu baadaye, bado nina muda sijaishia katika Foolish Age,
Mapenzi ya Mungu, bali nina kazi nyingi ninazohitaji kuzifanya ili watu
wajue kwamba Lulu ana kipaji katika kazi ya sanaa na si kwamba niliingia
huku kwa bahati mbaya,” alisema Lulu.