KINANA ATINGA MASASI, ATAKA CCM IENDELEE KUIBANA SERIKALI JUU YA WAFUJAJI WA FEDHA ZA UMMA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/kinana-atinga-masasi-ataka-ccm-iendelee.html
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi na kuwaambia kila mtu kwenye utumishi wa serikali inabidi awajibike katika kufanikisha lengo na asiyeweza inabidi aachie ngazi alisema lazima tutangulize utumishi kwa umma.
Kadi
zilizorudishwa kutoka kwa wananchama wa vyama pinzani ambao kwa hiyari
yao leo wamerudi na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha
Chiungutwa wilayani Masasi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi ya aliyekuwa
Katibu Mwenezi wa chama cha NLD Taifa Ndugu Frank Rashid Maulano
aliyejiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji
cha Chiungutwa jimbo la Lulindi wilayani Masasi.
Wanachama
wapya waliojiunga na CCM pamoja na jumuiya zake wakinyoosha kadi zao
juu wakati wa kula kiapo cha uanachama mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Chiungutwa wilayani Masasi
mkoa wa Mtwara.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Machombe ambapo alipita kukagua ujenzi wa Bwawa la maji litakalo saidia kaya 150 kata ya Marika jimbo la Lulindi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Wananchi wa Kijiji cha Machombe wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara wakishangilia wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana anayetembea nchi nzima kukagua miradi mbali mbali ambayo zilikuwa ahadi za CCM.





