VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FULSA YA KUJIAJIRI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/vijana-watakiwa-kuchangamkia-fulsa-ya.html

Wanyakazi wa Bega kwa Bega Microfinance wakitoa huduma katika maonesho ya wiki ya vijana yanayoendelea mkoani Dodoma.
Aidha, Kampuni ya Godtec (T) Limited ya jijini Dares salaam kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, vijana na Utamaduni na Michezo imewawezesha vijana kufungua na kumiliki makampuni yao kujiajiiri na kuajiri vijana wengine.
Kupitia kampuni hiyo vijana wameunganishwa na kutengeneza makampuni ambayo yanawezeshwa kupata mikopo ya mitaji kwa ajili ya kazi za ujasiriamali.
Kwa upande mwingine ili kijana aweze kupata mkopo dhamana ni hisa za kampuni inayotaka kukopa. Kila kampuni inatakiwa kununua hisa kwenye Bega kwa bega Microfinance Company Limited ndio iweze kupata mkopo.