PICHA:UTAMBULISHO WA WASANII WA KIMATAIFA WALIOTUA DAR
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/pichautambulisho-wa-wasanii-wa.html
Mwanamuziki
TI wa Marekani akiingia kwenye ukumbi wa mkutano leo jioni hii kwenye
hoteli ya Seacleaf wakati yeye pamoja na Mwanamuziki Davido wa Nigeria
na wanamuziki wengine mbalimbali watakaoshiriki katika Tamasha la
Serengeti Fiesta ni Sheeedah walipoongea na waandishi wa habari kueleze
jinsi watakavyofanya mambo mamkubwa kwenye tamasha hilo linalofanyika
kwenye viwanja wa Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki
TI wa Marekani akisalimiana na Mwanamuziki Davido wa Nigeria wakati
walipokutana kwenye ukumbi wa mkutano tayari kwa kuongea na waandishi wa
habari kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw.
Steve Gannon.
Mwanamuziki
TI wa Marekani kulia akisikiliza kwa makini wakati mwanamuziki Davido
alipokuwa akizungumzia tamasha la Serengeti Fiesta ambapo pia ataimba
nyimbo zake.
Mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon akizungumzia
mafanikio ya Tamasha la Serengeti Fiesta wakati wa mkutano na waandishi
wa habari kushoto ni Mwanamuziki TI kutoka nchini Marekani na kulia ni
Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko SBL.
Mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon akifafanua
jambo katika mkutano huo kushoto ni Mwanamuziki TI kutoka nchini
Marekani.A

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Serengeti Fiesta Bw. Sebastian Maganga akifafanua jambo katika mkutano huo leo
Ephraim
Mafuru Mkurugenzi wa Masoko SBL akizungumzia burudani hizo katikati ni
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon
kushoto ni Mwanamuziki TI kutoka nchini Marekani..
Kutoka
kulia ni Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko SBL, Mkurugenzi mtendaji
wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw. Steve Gannon, Mwanamuziki TI kutoka
Marekani na Mwanamuziki Davido kutoka nchini Nigeria
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Clouds Media Bw. Joseph Kusaga akiwashukuru wanamuziki
wote watakaoshiriki katika kutoa burudani, Kampuni ya bia ya Serengeti
na vyombo vya habari kwa ushirikiano wao.
Mwanamuziki Victoria Kimani kutoka Nairobi nchini Kenya akizungumza katika mkutano huo
Mwanamuziki
Davido akitia neno katika mkutano huo huku mwanamuziki TI akisikiliza
kulia anayefurahia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti
SBL.
Mtu mzima TI akimwaga maneno yake kwa wanahabari










