Mwanafunzi auawa kikatili baada ya kubakwa, kuchinjwa shingo na kunyofolewa sehemu nyeti
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/mwanafunzi-auawa-kikatili-baada-ya.html
Mwanafunzi
wa shule ya msingi jijini Dar es Salaam mwenye umri wa miaka saba,
ameuawa kikatili baada ya kubakwa, kuchinjwa na kunyofolewa sehemu zake
za siri.
Mwanafunzi huyo wa darasa
la kwanza (jina linahifadhiwa), mwili wake ulikutwa umetupwa kwenye
shamba karibu na nyumbani kwao jana maeneo ya Mbezi Temboni, kata ya
Saranga.
Akisimulia tukio hilo,
mama wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa), alisema kuwa juzi baada ya
mwanawe kurejea toka shuleni alimuogesha na kumpa chakula majira ya saa
12 ya jioni.
Alisema baada ya
kumtayarishia chakula hicho, alitoka kidogo kuelekea Temboni na
aliporejea nyumbani hakumkuta mtoto wake na ndipo alipokwenda kwa
majirani kumtafuta.
Alisema mpaka saa 1 usiku
hawakufanikiwa kumuona mtoto huyo licha ya kuambiwa mara ya mwisho
alionekani akiwa anacheza na mtoto wa jirani yake.
Hata hivyo, alisema
alipokwenda kwa jirani kumuulizia kama wamemuona, alijibiwa kuwa
alionekana akiwa anacheza pembeni ya banda la nguruwe.
Alisema baada ya kufanya jitihada zote bila mafanikio aliamua kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi.
Aliendelea kusimulia kuwa
jana majira ya saa 2 asubuhi, alipata taarifa ya kuonekana kwa mwili wa
mtoto wake kwenye shamba moja lililopo karibu na nyumbani kwake.
Alisema mwili wa mwanawe umekutwa ukiwa umepandishwa nguo alizovaa juu huku nguo ya ndani ikiwa imevuliwa.
Aidha, sehemu zake za
siri zilikutwa zikiwa na uwazi kitendo kinachoonyesha kuwa aliingizwa
kitu na kunyofolewa baadhi ya viungo.
“Roho inaniuma sana
mwanangu jamani wamembaka na kisha kupanua sehemu zake za siri
inaonyesha kuna vitu vimechukuliwa na shingo yake wamemkata hata kwenye
kichwa chake karibu na paji la uso wamempiga kwa tofali,” alisema.
MMOJA WA WATUHUMIWA AKAMATWA
Baba wa mtoto huyo (jina
linahifadhiwa) akizungumza huku akitokwa na machozi alisema mmoja kati
ya watu waliofanya unyama huo amekamatwa.
"Pamoja na kukamatwa kwa mtuhumiwa lakini wameniachia kovu la huzuni," alisema.
Alisema mtuhumiwa huyo amewataja na wenzake wawili walioshiriki kufanya unyama huo ambao wanatafutwa na polisi.
Mwili wa mtoto huyo umehidhiwa katika Hospitali ya Tumbi na umeshafanyiwa uchunguzi.
Habari za uhakika ambazo
NIPASHE imezipata ni kuwa mtuhumiwa aliyekamatwa alikutwa na damu kwenye
chupi yake baada ya kukaguliwa na askari.
Mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuonekana mara ya mwisho na marehemu, aliwataja wenzake baada ya kubanwa na askari.
MAJIRANI WAZUNGUMZA
Akizungumza kwa niaba ya
majirani, Halima Omary, alisema taarifa za kuonekana kwa mwili wa mtoto
huyo walizipata kutoka kwa mmiliki wa shamba hilo baada ya kufika
shambani kwake asubuhi na kuona kishimo cha damu.
Anasimulia kuwa baada ya
kuona shimo hilo la damu alifuatilia michirizi ya damu hiyo shambani
hapo ambayo ilikuwa ikionyesha kama kuna mtu kaburuzwa.
“Baada ya mama huyo
kufuatilia damu hizo shambani kwake, ndipo alipokutana na maiti hiyo na
kuondoka kwenda kutoa taarifa kwa majirani na watu walipofika wakagundua
ni yule mtoto aliyekuwa akitafutwa baada ya kupotea,” alisema.
Alisema baada ya kufika
katika tukio hilo walimkuta mtoto huyo akiwa amejeruhiwa katika maeneo
ya sehemu zake za siri, kifuani, shingoni na kichwani.
Omary alisema kuna haja
ya serikali kuwachukulia hatua watu wenye mapori ambao hawayaendelezi
ili yasitumike kufanyia matukio kama hayo.
Naye Marry Machange
ambaye ni jirani wa marehemu aliitaka serikali iingilie kati suala hilo,
kwani katika Kata ya Saranga kuna mapori makubwa ambayo yanatakiwa
kuendelezwa hata kwa kujengwa zahanati kuliko kuachwa kuwa sehemu za
kufanyia mauwaji.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kata ya Saranga, Godwin Muro, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema alipata taarifa
za kupotea kwa mtoto huyo saa 12 jioni na kuamua kusambaza taarifa hiyo
katika kituo cha polisi cha Mbezi na kwa wananchi.
Mjumbe wa nyumba 10 shina
namba 25 katika eneo hilo, Asibwene Mwaipopo, alisema tukio hilo ni la
kinyama na halijawahi kutokea katika eneo hilo.
Naye Diwani wa kata ya
Saranga, Efyemu Kinyafu, alisema amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko
makubwa na kuwataka wananchi wasubiri majibu kutoka kwa polisi ambao
wanaufanyia uchunguzi mwili wa marehemu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Kinondoni, Camilius Wambura, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kueleza kuwa mtoto huyo katika maeneo ya shingoni amekatwa na kitu
chenye ncha kali.
“Kuna tatizo limeonekana
huenda ameingiliwa sana hivyo siwezi kuthibitisha kama sehemu zake
zimekatwa kuna mambo mengine hayapaswi kuzungumzwa ni ya kidaktari
zaidi,” alisema.
Kamanda Wambura alisema
mpaka sasa wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja na wengine wawili
wanaendelea kuwasaka ili hatua za kisheria zichukuliwe.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI