MAPENZI: WEMA NA BABA, DIAMOND NA MAMA
Tofauti na mastaa wengine ambao huandika majina ya wapenzi wao kwenye miili yao kuonesha jinsi wanalivyo na mapenzi nao, Nasibu Abdul ‘Di...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/mapenzi-wema-na-baba-diamond-na-mama.html
Tofauti
na mastaa wengine ambao huandika majina ya wapenzi wao kwenye miili yao
kuonesha jinsi wanalivyo na mapenzi nao, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Wema
Sepetu wamekuwa tofauti, Ijumaa limegundua.
Mastaa
hawa wameonyesha kuwa na mapenzi na wazazi wao ambapo mwandishi wetu
amebaini Diamond ameandika jina la mama yake mkononi huku Wema akiandika
jina la baba yake mkononi pia.
Wote
wamefanya hivyo kwenye mikono yao ya kushoto sambamba na uwepo wa tatoo
nyingine ambapo Wema ameandika ‘Daddy Sepetu’ na Diamond akaandika
Sandra…’
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wao wamedai huenda penzi la mastaa hao si la kudumu ndiyo maana wamekwepa kuandikana ili isije ikawa shida pale watakapomwagana.